NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

ALIYEWAHI kuwa mshambuliaji wa kikosi cha Yanga , Amisi Tambwe amesema mabosi wake hao wa zamani wakishindwa kumlipa pesa zake anazodai kwa wakati atarudi tena FIFA.

Mwaka jana ilitoka taarifa Shirikisho la Soka Duniani kupitia CAS limetoa amri kuwa Yanga wanapaswa kumlipa Dola 20,000 shilingi milioni 46.4 Tambwe ada ya usajili wa miezi mitatu .

Yanga walipewa siku 45 kukamilisha zoezi kuanzia Disemba 5 hadi kufikia Januari 19 Mwaka huu wanatakiwa kuwa wawe wamemlipa.

Akizungumza na Zanzibar Leo kwa njia ya simu,Tambwe alisema mpaka sasa hajawasiliana na mabosi wake hao lakini anaamini zoezi litakamilika.

Alisema kama Yanga watashindwa kufanya hivyo atalazimika kuwasiliana na wakili wake ambae yupo Ureno ili kuwajulisha FIFA.

Mimi sijajua wanawaza nini lakini hukumu kama ilivyosema siku 45 wawe wamenilipa, hivyo kama hawajanilipa basi nitawasiliana na mwanasheria wangu ana hapo atawajulisha FIFA kufikia maamuzi, “ alisema