TOKYO,JAPANI
TOKYO na mikoa mitatu jirani imeamua kuweka hatua za dharura kuanzia wiki hii hadi mwishoni mwa mwezi Januari ili kudhibiti ongezeko la visa vya virusi vya korona kwa kudhibiti matembezi ya watu.
Wakati wa mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao, magavana wa mikoa ya Tokyo, Saitama, Chiba na Kanagawa walikubaliana kutekeleza hatua zao kabla ya serikali kuu kutangaza hali ya dharura katika mikoa hiyo.
Tokyo na mikoa hiyo mitatu itawataka wakaazi kujizuia kwenda kwenye matembezi yasiyokuwa na ulazima .
Pia itaziomba sehemu zinazouza pombe kufunga kufikia saa mbili usiku na kuacha kutoa huduma ya pombe hadi saa moja jioni kwa kipindi cha siku nne kuanzia siku ya Ijumaa.
Kadhalika mikoa hiyo itaweka malengo husika ili kuyatia moyo makampuni kuhamasisha kikamilifu ufanyaji kazi nyumbani pamoja na kutofautisha saa za kazi na kuziomba sehemu za biashara kuzima taa mapema.