LONDON, England
KIPA wa timu ya England Newport County , Tom King, amevunja rekodi kwa ufungaji wa bao kutoka masafa ya mbali zaidi kwenye mechi rasmi ya soka.
Timu ya Newport County ilitangaza kwamba King alifunga bao kwa mkwaju kuelekea nyavu za timu pinzani kutoka umbali wa mita 96.01 na kuingia kwenye kitabu cha Guinness Book of Records.
Tom King alifunga bao ambalo liliifanya timu yake iongoze kwa bao 1-0 katika dakika ya 12 ya mechi ya ligi waliyocheza dhidi ya Cheltenham Town mnamo Januari 19.
Mkwaju huyo aliopiga King ulipaa na kwenda moja kwa moja hadi lango la wapinzani ukampita kipa Josh Griffiths na kuingia wavuni.
Hapo awali, rekodi hiyo ya muda mrefu ya Guiness Book of Records ilikuwa ikishikiliwa na kipa Asmir Begovic aliyefunga bao kutoka umbali wa mita 91.9 kwenye mechi rasmi ya soka.