MCHAKATO mzima wa uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwenzi Novemba mwaka na umemalika ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, rais mteule Joe Biden anatarajiwa kulishwa kiapo mnamo Januari 20 mwaka huu.
Pamoja na kwamba kura zote zimeshahesabiwa zikiwemo zilizopigwa na wananchi pamoja na kura za wajumbe kuonesha kuwa rais wa sasa Donald Trump kushindwa, bado kiongozi huyo hajawahi kutamka kuwa ameshindwa.
Trump analalamika kuwa kumefanyika mchezo mchafu dhidi yake uliosababisha ashinde kwenye uchaguzi huo, hatuo hili sababisha kufundua mashitaka kupinga matokeo ya uchaguzi, lakini kesi zote zilitupwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.
Katika moja ya kituko kilichoripotiwa hivi karibuni nchini Marekani na kupewa kipaumbele kikubwa na vyombo vya habari ni hatua ya kudaiwa kuwa Trump alimpigia simu ofisa mkuu wa uchaguzi katika jimbo la Georgia kumtaka abadilishe matokeo ya uchaguzi.
“Nataka tu kupata kura 11,780,” Trump alimwambia katibu wa chama cha Republican Brad Raffensperger katika jimbo hilo kwenye mazungumzo kwa njia ya simu yaliyorekodiwa na kutolewa na gazeti la Washington Post.
Katika mazungumzo hayo Raffensperger alisikika akijibu kuwa matokeo ya uchaguzi ya Georgia yalikuwa sawa na ni vigumu kubadilishwa.
Matokeo katika jimbo hilo yalimpa ushindi Joe Biden pamoja na majimbo mengine muhimu na kumuwezesha kupata kura 306 za wajumbe dhidi ya kura 232 za Trump.
Majimbo yote 50 yamethibitisha matokeo ya uchaguzi huo baadhi ya vituo ikiwa ni baada ya kura kuhesabiwa tena au pia kwasababu ya kesi zilizowasilishwa mahakamani kupinga matokeo.
Hadi kufikia sasa, Marekani imetupilia mbali kesi 60 zilizokuwa zimewasilishwa kupinga ushindi wa Biden na inatarajiwa bunge litaidhinisha rasmi matokeo ya uchaguzi huo.
Wapiga kura huko Georgia wanatarajiwa kupiga tena kura kuchagua maseneta wawili wa jimbo hilo na matokeo ya uchaguzi huo huenda yakaweka sawa jinsi nguvu ya uongozi itakavyokuwa katika bunge la seneti.
Ikiwa washindani wawili wa chama cha Democrat watashinda, kunamaanisha kwamba kutakuwa na idadi sawa ya wabunge wa vyama vya Republican na Democratic na makamu mteule wa chama cha Democratic Kamala Harris ndiye atakayekuwa na usemi katika kura ya kufanya maamuzi.
Nini kilichotokea katika simu ya Trump? Katika kipande kilichotolewa na gazeti la Washington Post, kilimnukuu Trump akisema pengine njia nyingine ni kumshawishi na kumshinikiza katibu wa jimbo la Georgia.
Alisisitiza kuwa ameshinda uchaguzi katika jimbo la Georgia na kumuambia Raffensperger kwamba hakukuwa na ubaya wowote kusema kuwa “mumehesabu kura tena”.
Raffensperger alijibu kwa kusema: “Changamoto uliyonayo mheshimiwa rais ni kwamba takwimu ulizonazo wewe ni za uwongo.”
Baadaye katika simu hiyo, Trump alisema uvumi uliopo ni kuwa kura zilizopigwa kwa njia ya posta zimeharibiwa na mashine ya kupiga kura iliondolewa kutoka kaunti ya Fulton jimboni humo – dai ambalo wakili wa Raffensperger alisema sio sahihi.

Aidha, baadaye rais alimtishia ofisa huyo na kumtajia njia anazoweza kuchukua kisheria. “Unajua walichofanya na husemi lolote. Huo ni uhalifu. Huwezi kuacha hilo litendeke ukiwa kimya. Hiyo ni hatari kubwa kwako wewe na kwa Ryan, wakili wako,” Trump alisema.
Kisha akaitisha kura za ziada 11,780 – ambazo zitafanya awe na jumla ya kura 2,473,634 jimboni humo, moja zaidi ya kura alizopata Biden, 2,473,633 na kumuambia Raffensperger achunguze tena matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo.
“Unaweza kuyachunguza tena, lakini yafuatilie na watu ambao wanataka kupata majibu, wala sio wasiotaka kupata ufumbuzi,” alisema.
“Bwana Rais, unao watu wako wanaowasilisha taarifa na tuna watu wetu wanaowasilisha taarifa vilevile na kisha baada ya hapo yanafikishwa mahakamaani ambayo itafanya uamuzi,” Raffensperger aljibu. “Lazima tutetee nambari zetu na tunaamini kuwa takwimu zetu ziko sahihi.
Hata hivyo, Raffensperger hakutoa maelezo yoyote kuhusu ulaghai unaodaiwa na rais. “Hana taarifa yoyote!” Rais aliandika.
Bwana Raffensperger akajibu: “Kwaheshima, Rais Trump: Unachosema sio kweli. Ukweli utajitokeza.” Ikulu ya Marekani haijasema lolote kuhusu mazungumzo yaliyovuja.
Ofisa wa juu wa Democrat Adam Schiff aliesema kwa mara nyingine tena. “Jaribio la Trump kuingilia demokrasia liko wazi. Kupitia sauti iliyorekodiwa.”
Shirika la habari la Associated Press limemnukuu Bob Bauer, mshauri mkuu wa rais mteule Joe Biden, akisema kanda hiyo ni uthibitisho usiopingika kwamba Trump aliwashinikiza maafisa wa chama chake kubatilisha matokeo halali ya uchaguzi na badala yake kuhalalisha yaliyopatikana kwa njia za wizi.
Mwanasiasa wa Republican mwenye msimamo wa kati Adam Kinzinger ameandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema: “Bila shaka hii inachukiza. Kila mbunge anayefikiria kupinga matokeo ya uchaguzi huu, hawezi kufanya hivyo kwa nia moja.”
Je matokeo ya uchaguzi yataidhinishwa lini? Kuna mgawanyiko katika chama cha Republican baada ya maseneta 12 kusema kuwa hawatapiga kura kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden katika kikao cha bunge la seneti Januari 6.
Ted Cruz aliongoza maseneta 11 akiitisha kucheleweshwa kwa mchakato huo kwa siku 10 ili kuchunguza madai ya wizi wa kura.
Makamu wa rais Mike Pence, ambaye kama rais wa bunge la seneti anatarajiwa kusimamia kikao hicho na kumtangaza Biden mshindi alisema anaunga mkono hatua hiyo.
Pence hakurejelea madai ya wizi wa kura lakini mkuu wa wafanyakazi alisema Bwana Pence atashirikisha wengine kile anachosema ni “wasiwasi wa mamilioni ya wamarekani kuhusu wizi wa kura na udanganyifu”.
Seneta wa Missouri Josh Hawley pia alisema kuwa atapinga matokeo ya uchaguzi kwasababu ya madai ya ukosefu wa uadilifu.
Wakati huohuo, maseneta wanne akiwemo Mitt Romney wametia saini taarifa inayosema watapiga kura kuidhinisha ushindi wa Biden.