DONALD Trump amebakiwa na wiki moja kumalizia muhula wake mmoja wa miaka minne katika kuiongoza serikali ya Marekani, lakini sasa wingu zito limetanda bunge kutaka kumuoondoa madarakani pasi na kumstahamilia japo amebakisha siku chache.
Kilichofanya hadi wabunge kutaka kumuondoa madarakani Trump, ni baada ya wafuasi wake kuvamia bunge wiki moja iliyopita ambapo wabunge wamekasirishwa na hatua hiyo kwa kile wanachokieleza uvamizi wa wafusi hao umetokana na uchochezi alioufanya rais huyo.
Chama cha Democrats, ambacho kimeshinda kwenye uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka jana kupitia spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi, anataka Trump kuwajibishwa kutokana na ghasia alizozichochea zilizotokea Januari 6 mwaka huu.
Ingawa inaweza kuwa hatua hiyo ya kumuondoa ikawa imechelewa sana kabla ya muda wake kumalizika, bado wana nia ya kumuidhinisha kutopata haki zake kama rais mstaafu na kumzuia kujihusisha na shughuli nyingine za umma.
Kuna namna nyingi ambazo rais anaweza kutoa maagizo yake, lakini ni vigumu sana. Tuangalie mambo hayo kwenye marekebisho ya 25.
Viongozi wa juu wa Democrats – Spika Pelosi na Senata wa Democratic Chuck Schumer, wamemtaka makamu wa rais Mike Pence na baraza la mawaziri la Trump kumuondoa rais kutokana na uchochezi.
Pelosi anatafuta jibu katika bunge la Wawakilishi kwa kutoa wito kwa Pence kutumia marekebisho ya 25, katika kura ya kwanza iliyopangwa kupigwa Jumatatu ijayo.
Marekebisho ya 25, yanamruhusu makamu wa rais kukaimu nafasi ya rais wakati rais anaposhindwa kuendelea na majukumu yake, kwa mfano kama rais akipata matatizo ya kiafya au kiakili.
Pence atakuwa na saa 24 kama hatua hiyo itapita, kutumia marekebisho hayo kabla ya bunge kuanza mchakato wa kumuondoa Trump kupitia kura ya kutokua na imani naye.
Sehemu ya marekebisho hayo yamejadiliwa katika sehemu ya nne, ambayo yanaruhusu makamu wa rais na baraza lote la mawaziri kuthibitisha kuwa rais Trump ameshindwa kufanya majukumu yake.
Watahitajika kusaini barua kwa spika wa bunge na ofisa wa bunge kusema kuwa rais hayupo sawa na hawezi kuendelea na majukumu yake, hivyo inabidi kuondolewa madarakani, ikifikia hatua hiyo moja kwa moja Pence atachukua madaraka.
Rais anapewa nafasi kutoa maelezo ya maandishi na ikiwa atapinga kilichosemwa itakuwa ni jukumu la bunge kufanya maamuzi. Kura yoyote katika bunge la weneti na la Wawakilishi inayotaka rais kuondoka madarakani, inahitaji kupata theluthi mbili ya kura.
Hata hivyo, hakujakuwa na dalili zinazoonesha kuwa Pence, pamoja na angalau wabunge hata wanane wa baraza la mawaziri wanaunga mkono marekebisho hayo na kuna taarifa kuwa anapinga hatua ya kuondolewa madarakani bosi wake.
Kama makamu wa rais atashindwa kukaimu, Pelosi ameonesha dalili za kufanyika kwa zoezi la pili la kumuondoa madarakani Trump. Itakumbukwa kuwa Trump alishawahi kupigiwa kura ya kutokuwa na imani kutokana na madai ya kwamba alitafuta usaidizi Ukraine ili aweze kuimarisha uwezekano wa yeye kuchaguliwe tena.
Hata hivyo, wabunge wa Seneti walimuondolea makosa hayo. Trump anaweza kuwa rais wa kwanza katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa mara ya pili.
Kwa hilo kutokea suala la kuondolewa madarakani lazima lipelekwe katika bunge la Wawakilishi na kupigiwa kura. Kisha hoja hiyo itafikishwa katika bunge la seneti ambapo ni lazima ipitishwe na wabunge kwa kura za tatu ya nne ili rais aondolewe madarakani.
Kama akikutwa na hatia, wabunge wanaweza pia kupiga kura ya kumzuia Trump kushika wadhifa wowote ule katika ofisi ya umma.
Pia anaweza kupoteza marupurupu yake kama rais mstaafu chini ya sheria ya mwaka 1958 ambayo inajumuisha mafao, bima ya afya na ulinzi ambavyo vinagharamiwa na kodi ya raia.
Maamuzi kama hayo hayajawahi kufanyika katika historia ya Marekani na hakuna ishara kuwa Democrats wana idadi ya wawakilishi wanaoweza kuwa na nusu ya kura.
Taarifa fupi ya ndani iliyotolewa na kiongozi wa Republican Mitch McConnell anasema muda wa mapema zaidi ambao rais anaweza kuondolewa ni Januari 19, siku moja kabla ya muda wa Trump kuwa madarakani uishe.
Taarifa hiyo inasema kesi ya Trump inaweza kusikilizwa saa moja baada ya kuondoka madarakani au siku moja baadaye.
Lakini viongozi waandamizi katika Bunge la Wawakilishi wanasema kuwa chama hicho huenda kisitume hoja yoyote ya kutokuwa na imani na rais katika bunge la Seneti hadi baada ya siku 100 za kwanza za Biden kuwa madarakani.
Jambo ambalo litamruhusu Biden kuunda baraza lake la mawaziri na kuanza sera zake muhimu ikiwa ni pamoja na kukabiliana na virusi vya corona.
Wataalamu wa katiba wamegawanyika katika kukubali kama zoezi la kumuondoa rais madarakani linaweza kuendelea katika bunge la seneti iwapo tayari rais amemaliza muda wake.
Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu vyanzo ambavyo havikutajwa, na kusema kwamba Trump amependekeza kwa wasaidizi wake kuwa anafikiria kujipa msamaha siku zake za mwisho za urais.
Rais tayari anachunguzwa katika kesi kadhaa ikiwemo kuhusiana na suala la kama alipotosha mamlaka ya kodi, benki na washirika wa kibiashara katika jimbo la New York.
Je inawezekana rais kujisamehe? Kwa kifupi hilo halijulikani kwasababu hakuna rais aliyetangulia ambaye amewahi kutoa msamaha wa aina hiyo.
Baadhi ya wataalamu wa sheria wamewahi kusema hilo haliwezekani wakirejea tamko lililotolewa na wizara ya sheria siku kadhaa kabla ya Richard Nixon kujiuzulu kuwa asingeweza kujiwekea mwenyewe msamaha kwa kuzingatia kanuni moja ya msingi kwamba hakuna yeyote ambaye anaweza kuwa hakimu katika kesi yake mwenyewe.
Ingawa kuna uwezekano kuwa ni kidogo tu ambao wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais katika Bunge la Wawakilishi kama ilivyotokea mwaka 2019 – inaonekana kuwa lisiloaminika kwamba theluthi mbili ya wabunge wa Seneti wanaweza kupiga kura ya kumuondoa rais.
Ni idadi ndogo tu ya maseneta wa Republican ambao wametoa wito Trump kujiondoa na kusema wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, lakini hakuna ambaye amesema kwamba watamhukumu kwa kufanya makosa.
Ingawa kumekuwa na taarifa kwamba suala hilo limejadiliwa katika ngazi ya juu, mawaziri wawili wamepinga vitendo vya Trump na wamejiuzulu na wale waliosalia ni vigumu sana kwao kuungana na wanaotaka kumchukulia hatua ya kumuondoa madarakani.