Jesse Lingard
MANCHESTER United imemuongezea kandarasi ya mwaka mmoja kiungo wa England, Jesse Lingard na sasa kandarasi ya mchezaji huyo itakamilika 2022. (Sky Sports).

Georginio Wijnaldum
KIUNGO wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30), ameiambia Liverpool kwamba anataka kutia saini mkataba mpya, lakini, pande hizo mbili bado zinatofautiana kuhusu masharti ya mkataba huo. (90 Min).

Sami Khedira
KIUNGO wa Juventus na Ujerumani, Sami Khedira (33) ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu atazungumza na Everton kuhusu uhamisho. (Mail).

Isco
ARSENAL inajiandaa kumnunua kiungo wa Real Madrid na Hispania Isco kwa kipindi cha msimu uliobakia, lakini, wanasubiri kuona iwapo klabu hiyo ya itamuachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kati kati ya kampeni yao. (Goal.com).

Sokratis Papastathopoulos
BEKI wa Arsenal na Ugiriki, Sokratis Papastathopoulos (32), anakaribia makubaliano kuhamia katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (Takvim).

Eric Garcia
BEKI wa Hispania, Eric Garcia (19), ameafikiana na Barcelona kujiunga na wababe hao wa ‘La Liga’ katika mkataba wa miaka mitano kufuatia kukamilika kwa kandarasi yake na Manchester City mwezi Juni na Barcelona huenda wakakamilisha uhamisho huo mwezi Januari. (CBS Sports).

Demarai Gray
WINGA wa Leicester City, Demarai Gray (24), ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu ananyatiwa kama mchezaji huru na klabu za Roma na Benfica. (Sun).

Mino Raiola
WAKALA, Mino Raiola amepinga madai kwamba mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Haaland (20), atajiunga na Barcelona iwapo Emili Rousaud atashinda uchaguzi wa urais katika klabu hiyo. (90 Min).

Erling Haaland
KLABU ya Real Madrid ina matumaini itamsaini Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund. (AS).

Mohamed Simakan
CHELSEA imeungana na AC Milan na Nice katika kuonyesha azma ya kutaka kumsajili beki wa Ufaransa na Strasbourg, Mohamed Simakan (20). (Le10 Sport).

Mikel Arteta
MENEJA wa Arsenal, Mikel Arteta ana wasiwasi kwa meneja mwenza wa West Brom, Sam Allardyce kuhusu virusi vya ‘corona’, lakini, amesema, Ligi Kuu ya England haihitaji mapumziko ya wiki mbili licha ya ongezeko la maradhi hayo katika klabu. (Evening Standard).