Xherdan Shaqiri
LIVERPOOL wamebadilisha msimamo wao juu ya winga wa Uswisi, Xherdan Shaqiri (29), na hawatamruhusu kuondoka mwezi huu. (Liverpool Echo).

Jadon Sancho
MANCHESTER United wanaamini wanaweza kumsajili winga wa England mwenye umri wa miaka 20, Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund kwa chini ya pauni milioni 100 mwaka huu. (Dakika 90)

Dele Alli
KOCHA mpya wa Paris St-Germain, Mauricio Pochettino, amehusishwa na wachezaji wake wawili wa zamani wa Tottenham, kiungo wa England Dele Alli (24), na mchezaji wa Inter Milan raia wa Denmark, Christian Eriksen (28). (AS).

Ryan Christie
ARSENAL imeungana na klabu nyingi za Ligi Kuu ya England zinazovutiwa na kiungo wa Celtic wa Scotland, Ryan Christie (25), na wanatumai beki wao wa zamani wa kushoto wa Bhoys, Kieran Tierney (23), anaweza kumshawishi aende Emirates. (90 Min).

Rob Holding
MLINZI wa Arsenal, Muingereza Rob Holding (25), anakaribia kukubali kandarasi mpya ya muda mrefu, kumaliza matarajio ya timu za juu zinazotaka kumchukuwa kwa mkopo. (Telegraph).

Jose Mourinho
MENEJA, Jose Mourinho, amesema, itakuwa mshangao mkubwa ikiwa Tottenham watajishughulisha na dirisha la Januari na amesisitiza kwamba hatomuuliza mwenyekiti, Daniel Levy, kuongezewa nguvu. (Standard).

Roy Hodgson
MENEJA wa Crystal Palace, Roy Hodgson, amesema, hana wasiwasi na uvumi mpya juu ya siku zijazo za Wilfried Zaha huku AC Milan na Paris St-Germain zikiwa timu za hivi karibuni kuhusishwa na mshambuliaji huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 28. (Mail).

Zinedine Zidane
KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amepuuza maoni kwamba kiungo wa Croatia, Luka Modric (35), beki wa Hispania, Sergio Ramos (34), na mchezaji mwenzake wa Hispania, Lucas Vazquez (29), wataondoka klabuni. (Team Talk).

Frank Lampard
KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard ana maoni kwa dirisha la uhamisho la Januari, lakini, anaweza kulazimika kupunguza ukubwa wa kikosi chake kupitia mauzo na mikopo kabla ya kutumia. (Goal).

DeAndre Yedlin
NYOTA wa Marekani, DeAndre Yedlin (27), bado anaweza kuwa na jukumu la kucheza huko Newcastle msimu huu, licha ya mazungumzo juu ya kuondoka Januari na maslahi kutoka kwa miamba ya Uturuki ya Trabzonspor.(Newcastle Chronicle).

Graziano Pelle
JUVENTUS inafikiria kumchukua mshambuliaji wa zamani wa Italia wa Shandong Luneng mwenye umri wa miaka 35, Graziano Pelle, ambaye amekuwa akihusishwa na West Ham. (Goal).

Nuno Espirito Santo
MENEJA, Nuno Espirito Santo, amesema, ‘Mbwa mwitu’ wapo tayari kufanya maamuzi” katika dirisha la uhamisho la Januari. (Express & Star).