Sergio Ramos
MANCHESTER City wanachunguza hali ya beki, Sergio Ramos, katika klabu ya Real Madrid wakiwa na lengo la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kutoka Hispania atakayekuwa huru msimu huu. (ESPN).

Kevin de Bruyne
KIUNGO wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne (29), anatarajiwa kukataa ofa ya kwanza ya kandarasi ya Manchester City na ana wasiwasi kuhusu kasi ya klabu hiyo katika mazungumzo ya kumpatia kandarasi mpya ya miaka mitano. (Times).

Dele Alli
KLABU ya Tottenham haipo tayari kumuuza ama kumtoa kwa mkopo kiungo wa England, Dele Alli (24), mwezi huu, lakini, kipa wa Argentina, Paulo Gazzaniga (29) na beki wa England, Danny Rose (30) wataruhusiwa kuondoka. (Sky Sports).

Frank Lampard
CHELSEA ipo tayari kumpatia muda zaidi kocha, Frank Lampard, lakini, hali hiyo inaendelea kuchunguzwa huku Thomas Tuchel , Max Allegri , Brendan Rodgers na Ralph Hasenhuttl wakifikiriwa kama mameneja wabadala iwapo atafutwa kazi. (Independent).

Andriy Shevchenko
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Andriy Shevchenko ambaye kwa sasa ndiye kocha wa timu ya taifa ya Ukraine pia anafikiriwa kujaza pengo la Lampard iwapo atafutwa. (Le10 Sport).

Mohamed Elneny
ARSENAL haina mpango wa kumuuza, Mohamed Elneny (28), katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku kukiwa na azma kutoka klabu ya Spurs. (Football London).

Mesut Ozil
ARSENAL wameipatia ofa Juventus kiungo wao wa kati, Mesut Ozil (32) katika wiki za hivi karibuni, lakini, mabingwa hao wa Italia wanamuona mchezaji wa Sweden, Dejan Kulusevski (20) kama mwenye kipaji kwa siku zijazo katika safu hiyo. (CBS Sports).

Emi Buendia
ARSENAL inachunguza hali ya kiungo wa Argentina, Emi Buendia, lakini, bado hawajawasilisha ombi rasmi la mchezaji huyo wa Norwich mwenye umri wa miaka 24.(Football London).

Marcos Rojo
BEKI wa Manchester United na Argentina, Marcos Rojo (30), amefanya mazungumzo na klabu ya Boca Juniors nyumbani kwao, ijapokuwa bado hawajaafikiana kuweka kandarasi. (Mail).

Eric Bailly
KIWANGO cha mchezo wa beki wa Ivory Coast, Eric Bailly (26), kinaweza kuishawishi Manchester United kutotafuta beki mwengine wa kati mwezi huu. (Manchester Evening News).

Georginio Wijnaldum
WACHEZAJI wanaolengwa na Barcelona ni kiungo wa kati wa Liverpool na Uhalonzi Georginio Wijnaldum (30), beki wa kati wa Manchester City na Hispania, Eric Garcia (19), na mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi, Memphis Depay (26).(Goal).

Moise Kean
KLABU ya Paris St-Germain imeanza mazungumzo na Everton kubadilisha kandarasi ya mkopo ya mshambuliaji wa Italia, Moise Kean kwa mkataba wa kudumu wenye thamani ya pauni milioni 31. (Sky Sports).