Emi Buendia
ARSENAL imehusishwa na kiungo wa kati wa Norwich City, Emi Buendia (24), lakini, kuna uwezekano mdogo ikamsajili raia huyo wa Argentina, kwa sababu ya ukosefu wa fedha. (Mirror).

Mesut Ozil
KIUNGO wa Arsenal raia wa Ujerumani, Mesut Ozil (32), anafanya mazungumzo na DC United kuhusu kuhamia klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Marekani. (Football London)

Sergio Ramos
BEKI wa Hispania, Sergio Ramos (34), amekataa ofa ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja na Real Madrid, ambayo haitaki kwenda kinyume na sera yao ya kutoa makubaliano zaidi ya 30 ya muda huo kwa wachezaji wake.(Goal).

David Alaba
REAL Madrid ipo katika nafasi nzuri ya kumsajili mlinzi wa Bayern Munich raia wa Austria David Alaba, ambaye hajakuwa kwenye mkataba wowote msimu huu, lakini, Liverpool imeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo (28). (Guardian).

Pep Guardiola
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, ana uhakika wa asilimia mia moja kuwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne (29), atatia saini makubaliano mapya na klabu hiyo, licha ya taarifa kuwa mchezaji huyo, amepanga kukataa ofa ya mkataba wao. (Sky Sports).

Harry Kane
KLABU ya Tottenham Hotspurs imesitisha mazungumzo na washambuliaji wa England, Harry Kane (27), na Son Heung-min (28) wa Korea Kusini kutokana na janga la virusi vya ‘corona’. (Evening Standard).

Kingsley Coman
WINGA wa Ufaransa, Kingsley Coman, amehusishwa na Manchester City na Manchester United, lakini, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amesema, yuko sawa na mwenye furaha Bayern Munich. (Bild).

Graziano Pelle
WEST Ham United huenda ikaanza kutafuta mbinu za kumsajili mshambuliaji wa Italia, Graziano Pelle, ambaye tu ndio ameondoka klabu ya Shandong Luneng ya Chinese Super League ikiwa itashindwa kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King (28). (Star).

Marko Arnautovic
KLABU ya West Ham imeamua kutomsajili mshambuliaji wa Austria, Marko Arnautovic (31), aliyehama klabu hiyo na kujiunga na Shanghai SIPG ya Chinese Super League kwa sababu itakuwa gharama. (Mail).

Dani Ceballos
KIUNGO wa Real Madrid, Dani Ceballos (24), ambaye yuko Arsenal kwa mkopo ana matumaini ya kurejea kwa klabu yake ya utotoni na kushiriki katika kikosi cha kwanza. (Cadena Ser).

Ronald Koeman
KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman, amesema, ametengeneza orodha ya wachezaji “ambao itakuwa bora wakipatikana”. (Marca).

Ben Pearson
KLABU ya Brentford inamnyatia kiungo wa kati wa Preston North End, Ben Pearson (26), ambaye mkataba wake na klabu ya Deepdale unakamilika msimu huu. West Bromwich Albion na Celtic pia zimehusishwa na mchezaji huyo. (Mail).

James Beattie
ALIYEKUWA mshambuliaji wa England na Southampton, James Beattie ni miongoni mwa wagombea wanaopigania kuchukua nafasi ya kocha wa timu ya Fleetwood Town baada ya Joey Barton kuondoka. (Mail).