Moise Keane
KLABU ya Everton inatarajia kupokea ofa za Moise Keane (20) kutoka PSG ambapo mshambulaji huyo wa Italia yuko katika mkopo, lakini, pia Everton haina haraka kuamua kuhusu hatma yake ya baadaye. (Liverpool Echo).

Georginio Wijnaldum
MAZUNGUMZO mapya ya kandarasi kati ya Liverpool na kiungo wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30), yamegonga mwamba. (Sky Sports).

Agusti Benedito
MGOMBEA wa urais katika klabu ya Barcelona, Agusti Benedito, amesema, hafikirii kwamba Lionel Messi (33), ataongeza mtakaba wake katika klabu hiyo unaoisha mwezi Juni 2021. (Goal).

Lionel Messi
MANCHESTER City inaamini wapo mbele ya mstari kumsaini, Lionel Messi iwapo mshambuliaji huyo wa Argentina ataondoka Barcelona katika majira ya joto. (Telegraph).

Mesut Ozil

KIUNGO wa Arsenal na Ujerumani, Mesut Ozil (32), amekubali mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (DHA).

Amad Diallo
KLABU ya Atalanta inapania kumtoa kwa mkopo winga wake wa Ivory Coast, Amad Diallo (18), kwenda Manchester United hadi mwishpo wa msimu. (Manchester Evening News).

Paul Pogba
MANCHESTER United itamuuza kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba (27), msimu wa joto baada ya kukubali kuwa hatatia saini mkataba mpya. (Sunday Mirror).

Jadon Sancho
MANCHESTER United haijaamua ikiwa itamfuatilia winga wa England, Jadon Sancho (20), baada ya meneja, Ole Gunnar Solskjaer kuvutiwa na mchezaji mwenzake wa Borussia Dortmund mshambuliaji wa Norway, Erling Braut Haaland. (Sunday Mirror).

Mauricio Pochettino
MENEJA mpya wa Paris St-Germain, Mauricio Pochettino ana matumaini mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe (22), atatia saini mkataba mpya licha ya kunyatiwa na Liverpool. (AS).

William Saliba
KIUNGO,William Saliba yuko tayari kupunguziwa mshahara Ili kuondoka Arsenal huku klabu kadhaa zikitarajiwa kumng’ang’ania mlinzi huyo Mfaransa aliye na umri wa miaka 19, dirisha la uhamisho wa Januari litakapofunguliwa. (L’Equipe).

Hamza Choudhury
KLABU ya Newcastle ni miongoni mwa vigogo vinavyopewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Leicester, Hamza Choudhury (23). (Newcastle Chronicle).

Ozan Kabak
KLABU ya Crystal Palace ni miongoni mwa vigogo vinavyomtaka mlinzi wa Schalke, Mturuki Ozan Kabak (20). (Mail).

Fikayo Tomori
MENEJA wa Newcastle, Steve Bruce, anapania kumsajili mlinzi wa Chelsea, Fikayo Tomori (23). (Mail).

Olivier Giroud
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa, Olivier Giroud (34) ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda West Ham, amesema angelipendelea kusalia Chelsea na kushinda mataji. (Sky Sports).