Dario Sarmiento
MANCHESTER City inakaribia kumsaini ‘Messi mdogo’ Dario Sarmiento. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 winga wa Argentina anaichezea klabu ya Estudiantes katika ligi ya nchi hiyo. (Talksport).

Mesut Ozil
MENEJA wa Fernabahce, Erol Bulut, amesema, hali kuhusu uwezekano wa klabu hiyo kumsaini kiungo mchezeshaji wa Arsenal na Ujerumani, Mesut Ozil (32), itakuwa wazi katika siku chache zijazo. (Mirror).

Brandon Williams
MENEJA wa Newcastle, Steve Bruce, anataka kuwasainiwa wachezaji watatu wa England wanaochezea Manchester United kwa mkopo mwezi huu na amezungumza kwa muda mrefu na klabu yake ya zamani kuhusu winga, Brandon Williams (20), beki Phil Jones (28), na kiungo, Jesse Lingard (28). (90min).

Djibril Sidibe
KLABU ya Newcastle pia imewasiliana na Monaco kuhusu beki wa Ufaransa, Djibril Sidibe (28). (Foot Mercato).

Sean Dyche
MENEJA wa Burnley, Sean Dyche, ametaka chanjo ya ‘corona’ kuharakishwa katika soka huku fedha zinazohifadhiwa kuwapima wachezaji zikipelekwa katika idara ya afya. (Guardian).

Donny van de Beek
KIUNGO wa Manchester United na Uholanzi, Donny van de Beek huenda akaondoka kulingana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Dimitar Berbatov. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameanzishwa katika mechi mbili za ligi msimu huu baada ya kusainiwa kwa dau la pauni milioni 35 mwezi Septemba. (Betfair).

Sergio Romero
KIPA wa Manchester United na Argentina, Sergio Romero (33), anatarajiwa kurudi katika klabu hiyo wiki ijayo huku mazungumzo kuhusu hatma yake yakiendelea. (Sky Sports).

Roman Abramovich
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich amepeana baadhi ya vyumba vya hoteli ya Stamford Bridge kwa wafanyakazi wa Afya NHS kwa mara nyengine. (Independent).

MENEJA wa Watford, Xisco Munoz, ameambia wachezaji wake ‘kucheza kama wanyama’ wakati wa mechi ya FA dhidi ya Manchester United (Evening Standard).

Ainsley Maitland-Niles
KLABU ya Atletico Madrid inajaribu kumsajili beki wa Arsenal na England mwenye umri wa miaka 23, Ainsley Maitland-Niles kwa mkopo mwezi Januari. (Mail).

Kylian Mbappe
KUTIMULIWA kwa kocha wa PSG, Thomas Tuchel, kumeathiri matumaini ya Real Madrid kumsaini mshambuliaji, Kylian Mbappe kutoka klabu hiyo ya ‘Ligue 1’.(AS).

Marcos Alonso
BEKI wa kushoto wa Chelsea, Marcos Alonso, pia analengwa na Atletico Madrid, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akikosa fursa ya kukichezea kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya Stamford Bridge msimu huu. (El Chiringuito).

David Alaba
MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, anataka kusaini beki wa kati mwaka ujao, lakini, hatajiunga katika kinyanganyiro cha kumsaini beki wa Austria, David Alaba (28), ambaye kandarasi yake inaisha mwisho wa msimu. (Telegraph).

Hakan Calhanoglu
MENEJA wa AC Milan, Stefano Pioli anataka kiungo wa kati wa Uturuki, Hakan Calhanoglu ambaye amehusishwa na Manchester United kusalia katika klabu hiyo huku mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiendelea. (Goal).

Marten de Roon
MANCHESTER City na Tottenham zinamchunguza kiungo wa Atalanta na Uholanzi mwenye umri wa miaka 29, Marten de Roon ambaye aliwahi kuichezea Middlesbrough mapema akianza kucheza soka. (90 Min).

Cenk Tosun
MENEJA wa Feyenoord, Dick Advocaat, amefutilia mbali hatua ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Everton na Uturuki, Cenk Tosun (29). (FC Update).

Shkodran Mustafi
BARCELONA imepinga madai kwamba ina azma ya kumsajili beki wa Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 28, Shkodran Mustafi. (Mundo Deportivo).

Moises Caicedo
CHELSEA imejiunga na Manchester United katika kuonesha azma ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Ecuador, Moises Caicedo (19), anayeichezea klabu ya Independiente del Valle. (Mail).

Fabian Ruiz
KLABU ya Napoli itasikiliza ofa za kiungo wa Hispania, Fabian Ruiz baada ya mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na mchezaji huyo. (Calciomercato).