MESUT OZIL
KIUNGO wa Arsenal Mesut Ozil yupo kwenye mazungumzo ya kujiunga na kabu ya Uturuki ya Fenerbahce kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Ingawaje washika bunduki hao wamesema hawataki kulipa sehemu ya pauni 350,000 kwa wiki mshahara huo ikiwa uhamisho utafanyika. (Guardian)
MAURICIO POCHETTINO
BOSI wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anataka kumsaini mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, katika uhamisho huru msimu huu wakati mchezaji huyo 32 mkataba wake utakapo malizika hapo Manchester. (Mirror)
JULIAN BRANDT
ARSENAL wanahusishwa na mpango wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 24 Julian Brandt mwezi huu, na klabu hiyo yake ya Bundesliga ipo tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Bild – in German)
EDER MILITAO
TOTTENHAM inavutiwa na kutaka kumsaini beki wa Real Madrid na Brazil Eder Militao, 22. (Mundo Deportivo – in Spanish)
TOBY ALDERWEIRELD
BEKI wa kati wa Spurs na Ubelgiji Toby Alderweireld, 31, anawindwa na PSV Eindhoven. (De Telegraaf – in Dutch)
HARRY WINKS
VALENCIA imefanya mazungumzo na Tottenham juu ya uhamisho wa kiungo wa England Harry Winks. (AS – in Spanish)
OLE GUNNAR SOLSKJAER
MENEJA wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema kipa Sergio Romero, 33,na beki Marcos Rojo, wote watacheza timu ya taifa ya Argentina, wanaweza kuondoka klabuni hapo mwezi huu. (Manchester Evening News)
EDDIE NKETIAH
WEST HAM wamemtambua mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 21, kama chaguo la kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Sebastien Haller kujiunga na Ajax ya Uholanzi. Mshambuliaji wa Bournemouth wa Norway Joshua King, 28, na Stade Reims mwenye umri wa miaka 24 na mshambuliaji wa Senegal Boulaye Dia pia wanatakiwa na klabu hiyo.(London Evening Standard)
BERNARD
EVERTON haijafanya mazungumzo na klanu ya Itali ya Roma kuhusu kumuuza kiungo wa miaka 28 wa Brazil Bernard, alisema meneja Carlo Ancelotti. (Liverpool Echo)
CARLO ANCELOTTI
LAKINI Ancelotti amefungua mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji Moise Kean kwa Paris St-Germain endapo mabingwa wa Ufaransa watataka kubadilisha mpango wa mkopo wa kijana huyo wa miaka 20 kwa uhamisho wa kudumu.(Guardian)
BRANDON WILLIAMS
BEKI wa kushoto wa Manchester United, Brandon Williams angependa kuhamia kwa mkopo kwa klabu nyingine ya Ligi Kuu, huku Newcastle United na Southampton zikiwa zimehusishwa na Muingereza huyo wa miaka 20. (Manchester Evening News)
FILIP BENKOVIC
CELTIC inafanya mazungumzo na Leicester City kuhusu kumsajili beki wa kati wa Croatia Filip Benkovic, 23, ambaye alichezea mabingwa wa Scotland kwa mkopo mnamo 2018-19. (Sky Sports)
JASON KNIGHT
LEEDS wanavutiwa na viungo wa kati wa miaka 19 wa Derby County Jason Knight na Louie Sibley. (Football Insider)