Dayot Upamecano
BEKI wa RB Leipzig na Ufaransa, Dayot Upamecano (22), anatakiwa na Bayern Munich, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikijiunga na Chelsea na Manchester United katika kumtafuta beki huyo. (Marca).

Eder Militao
KLABU ya Tottenham huenda ikamsajili beki mwenye umri wa miaka 22 raia wa Brazil, Eder Militao, anayesakwa na Roma, AC Milan na Inter kwa mkopo kutoka Real Madrid ikiwa na mbadala wa kumnunua kwa mkataba wa kudumu. (Corriere dello Sport).

Nicolas Gonzalez
JOSE Mourinho imeungana na Leeds na Juventus katika kumsaka winga wa Stuttgart, Nicolas Gonzalez (22), huku mchezaji huyo wa Argentina akilengwa katika dirisha la uhamisho la majira ya joto. (The Athletic).

Harry Winks
VALENCIA ina azma ya kumsajili kiungo wa kati wa Spurs na England mwenye umri wa miaka 24, Harry Winks kwa mkopo . (Football London).

Moises Caicedo
KLABU ya Brighton ina imani wataishinda Newcastle United katika kumsaini kiungo wa kati wa Ecuado, Moises Caicedo kutoka klabu ya Indipendiente del Valle. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa akilengwa na Manchester United.(Talksport).

Steven N’Zonzi
KIUNGO wa Ufaransa na mshindi wa Kombe la Dunia, Steven N’Zonzi, huenda mkataba wake wa mkopo katika klabu ya Rennes ukakatizwa baada ya kuhusishwa na uhamisho wa Arsenal na Everton . (Foot Mercato).

Moussa Dembele
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa na Lyon, Moussa Dembele (24), anakaribia uhamisho wa kwenda Atletico Madrid baada ya kukataa kutimkia West Ham. (Telefoot).

Emi Buendia
ARSENAL hailengi tena kumsajili kiungo wa Norwich, Emi Buendia baada ya klabu hiyo kuweka dau la pauni milioni 40 kumuuza mchezaji huyo wa Argentina. (Express).

Tiemoue Bakayoko
KIUNGO wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Stamford Bridge huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiendelea kuivutia Napoli ambapo yupo kwa mkopo. (Star).

Jetro Willems
BEKI wa Uholanzi, Jetro Willems anaonekana huenda akarudi katika klabu ya Newcastle United kutoka Eintracht Frankfurt, hatua hiyo inajiri baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuhusishwa na kurejea klabu hiyo ya Tyneside. (Chronicle).

Fredrik Andre Bjorkan
KLABU ya Leeds United imehusishwa na beki wa Norway anayetafutwa na Sampdoria mwenye umri wa miaka 22, Fredrik Andre Bjorkan. (La Repubblica).

Jonjoe Kenny
KLABU ya Burnley inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsaini beki wa Everton mwenye umri wa miaka 23, Jonjoe Kenny, baada ya kushindwa hapo awali kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21. (Football Insider).

Gianluca Scamacca
JUVENTUS ipo katika mazungumzo na Sassuolo kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Italia mwenye umri wa miaka 22, Gianluca Scamacca, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Serie A’ ya Genoa. (Goal).