Odion Ighalo
MSHAMBULIAJI wa Nigeria, Odion Ighalo (31), anafikiria kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS . Uhamisho wake wa mkopo Manchester United kutoka klabu ya China ya Shanghai unakamilika mwisho wa mwezi huu. (ESPN).
Gareth Bale
KLABU ya Tottenham huenda isiongeze mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale (31), kutoka Real Madrid kwa msimu wa 2021-22. (Times).
Tariq Lamptey
BEKI wa Brighton, Tariq Lamptey (21), anakaribia kuandikisha mkataba wa kandarasi ya muda mrefu na klabu hiyo Ligi ya England. Bayern Munich ni miongoni mwa vigogo ambavyo vinahusishwa na uhamisho wa beki huyo wa timu ya wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 21 ya England. (Talksport).
Neymar
MSHAMBULIAJI wa Brazil, Neymar (28,) ameanza mazungumzo ya kuongeza kandarasi yake katika klabu ya Paris-St Germain. (Sky Sports).
Kim Min-jae
KLABU ya Tottenham na Chelsea zina azma ya kumsajili beki wa kati wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka 24, Kim Min-jae ambaye anaichezea Beijing Guoan ya China. (Mirror).
Boulaye Dia
WEST Ham inafikiria kumsajili mshambuliaji na wanamlenga nyota wa Reims na Senegal, Boulaye Dia, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akipatikana kwa dau la pauni milioni 15. (Eurosport).
David Brooks
ASTON Villa ina azma ya kumsaini kiungo wa Bournemouth na Wales, David Brooks (23), katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Talksport).
Dayot Upamecano
BEKI wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22, Dayot Upamecano, licha ya kwamba anaweza kuondoka katika majira ya joto kwa dau la pauni milioni 37.4, Liverpool, Chelsea, Manchester United na Bayern Munich ni miongoni mwa timu zinazomnyatia. (Guardian).
Frederic Guilbert
BEKI wa kulia wa Aston Villa na Ufaransa, Frederic Guilbert (26), amekataa uhamisho wa kweda katika klabu ya Uturuki ya Istanbul Basaksehir.(Football Insider).
Manor Solomon
ARSENAL ni miongoni mwa klabu zinazomchunguza winga wa klabu ya Shakhtar Donetsk na Israel, Manor Solomon (21), wakiwa na lengo la kuwasilisha ombi kwa klabu hiyo ya Ukraine katika majira ya joto. (Guardian).
Joan Laporta
JOAN Laporta, Victor Font na Toni Freixa ndio wagombea waliosalia katika kuwania wadhifa wa urais katika klabu ya Barcelona. Uchaguzi huo utafanyika Jumapili ya tarehe 24. (Mundo Deportivo).
Klaas-Jan Huntelaar
MSHAMBULIAJI wa Uholanzi, Klaas-Jan Huntelaar (37), huenda akarudi katika klabu ya Schalke. Mshambuliaji huyo aliondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani na kuhamia Ajax mwaka 2017 ambapo alihudumu kwa muda wa miaka saba. (Bild Sport).