DELE ALLI
KIUNGO wa Tottenham na England Dele Alli, 24, “anataka” kuhamia klabu bingwa ya Ufaransa Paris St-Germain Lakini mazungumzo baina ya timu hizo yamekuwa magumu. (Mwandishi Fabrizio Romano, kupitia Twitter)

GAETAN LABORDE
KLABU ya West Ham United inapima uwezekano wa kumsajili mshambuliaji kutoka Ufaransa Gaetan Laborde, 26, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Montpellier. (Telegraph )

CARLES TUSQUETS
KAIMU rais wa Barcelona Carles Tusquets amependekeza kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20, kwa euro milioni 8 kwa wagombea watatu wa urais wa klabu hiyo, lakini hakuna kinachoweza kufanyika kwa sasa kwa kuwa wote hakuwa na makubaliano. (Marca)

MEMPHIS DEPAY
MSHAMBULIAJI wa Uholanzi Netherlands Memphis Depay, 26, anasema yeye na mchezaji mwenzie wa klabu ya Lyon Houssem Aouar, 22, wanataka kuhamia katika “moja ya klabu tatu kubwa duniani.” Depay amekuwa akihusishwa na klabu ya Barcelona, huku kiungo kutoka Ufaransa Aouar anaripotiwa kunyemelewa na Arsenal. (Canal+)

SCOTT PARKER
KOCHA wa Fulham Scott Parker anasema anataka kusajili wachezaji na kumaliza usajili mapema katika dirisha la mwezi huu. (Evening Standard)

ANDRE VILLAS-BOAS
KOCHA wa Marseille Andre Villas-Boas amethibitisha kuwa kiungo Mfaransa Morgan Sanson, 26, ananyemelewa na klabu kadhaa za England zikiwemo; Arsenal, Aston Villa, Tottenham na West Ham.(Mail)

BEPPE MAROTTA
MKURUGENZI wa Inter Milan Beppe Marotta amesema kuwa klabu hiyo ipo vizuri kifedha lakini haitafanya uwekezaji wowote wa wachezaji katika dirisha la usajili la mwezi huu. (Sky Sport Italia)

GRANT MCCANN
KOCHA wa Hull City Grant McCann ametangaza kuwa mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Keane Lewis-Potter, 19, hauzwi, japo mazungumzo juu ya mkataba mpya baina ya Hull na mchezaji huyo yanaelekea kugonga mwamba. (Yorkshire Post)
