Nicolo Barella
LIVERPOOL na Tottenham wanaangalia uwezekano wa kufanya mkataba na kiungo wa kati wa Inter Milan Muitalia, Nicolo Barella (23). (Calciomercato).

Danny Ings
KLABU ya Tottenham wamepanga kumuhamisha mshambuliaji wa Southampton na England, Danny Ings (28). (Eurosport).

Ralph Hasenhuttl
MENEJA wa Southampton, Ralph Hasenhuttl, amesema hali ya kifedha ya klabu hiyo inamaanisha kuwa hawatoweza kuongeza mishahara ya wachezaji muhimu kama vile Ings. (Mirror).

Romelu Lukaku
MSHAMBULIAJI wa Inter Milan na Ubelgiji, Romelu Lukaku (27), hana haja ya kujiunga na Manchester City. (Express).

David Alaba
LIVERPOOL na Barcelona bado hawajakata tamaa ya kusaini mkataba na mlinzi wa Bayern Munich na Austria, David Alaba (28), licha ya kwamba Real Madrid wanakamilisha mkataba naye. (Sport1).

Facundo Medina
MANCEHESTER United wanaandaa dau la pauni milioni 11 kwa ajili ya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Lens na Argentina, Facundo Medina (21). (La Voix du Nord).

Jesse Lingard
KLABU ya Nice wametuliza nia yao ya kumchukua kiungo wa Manchester United na England, Jesse Lingard (28) kwa mkopo. (Sky Sports).

Dele Alli
KIUNGO wa Tottenham na England, Dele Alli (24), anaimani kuwa atasaini mkataba wake wa kuhamia Paris St-Germain katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari. (Sun).

Emi Buendia
KLABU ya Arsenal wameambiwa kiungo wa kati wa Argentina, Emi Buendia (24), ataondoka katika Norwich City wakati wa kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji. (Independent).

Douglas Luiz
MANCHESTER City wana chaguo la kumnunua tena mchezaji wa safu ya kati wa Aston Villa na Brazil, Douglas Luiz kwa pauni milioni 27.5 na muda wa chaguo hilo unakamilika msimu huu, lakini, meneja Pep Guardiola hatarajiwi kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (Birmingham Mail).

Gaetan Laborde
KLABU ya Montpellier imekataa dau kutoka kwa West Ham kwa ajili ya mshambuliaji Mfaransa Gaetan Laborde (26). (Guardian).

Diego Simeone
KLABU ya Atletico Madrid wanamtaka meneja, Diego Simeone, amesaini mkataba mpya, utakaomuwezesha kubakia katika klabu hiyo hadi mwaka 2024. (AS).

Martin Odegaard
KIUNGO wa Real Madrid Mnorway, Martin Odegaard (22), ameomba kuondoka katika klabu hiyo. (Marca).