Christian Benteke
KLABU ya Crystal Palace wapo wazi kumuuza, Christian Benteke baada ya kumsaini, Jean-Philippe Mateta.
Benteke amejitahidi kufikia matarajio tangu alipojiunga akitokea Liverpool mnamo 2016 na anaweza kutafuta changamoto mpya mahali pengine.(Goal).

Tyrick Mitchell
BEKI wa Crystal Palace, Tyrick Mitchell, anaivutia Arsenal na washika bunduki hao ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomtaka mchezji huyo mwenye umri wa miaka 21.
Mkataba wa sasa wa Mitchell unamalizika majira yajayo ya joto, lakini, Arsenal inaweza kuhangaika kupata makubaliano ya bei ya chini katika dirisha la Januari. (Goal).
but Arsenal may struggle to arrange a cut-price deal in the January window.

Kalidou Koulibaly
BEKI wa Napoli, Kalidou Koulibaly bado analengwa na Ole Gunnar Solskjaer huko Manchester United.
Kocha huyo mkuu raia wa Norway kwa muda mrefu amekuwa akimuhusudu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, na anaweza kuongeza azma yake baadaye mwaka wakati anatafuta kuimarisha chaguzi zake za ulinzi.(Marca).

Virgil van Dijk
LIVERPOOL wanapeana kipaumbele mkataba mpya wa Virgil van Dijk juu ya Mohamed Salah.
Van Dijk, ambaye kwa sasa hayuko nje ya uwanja na maumivu ya goti, amebakiza miaka miwili kumaliza mkataba wake wa sasa.(Goal).

Matej Vydra
KLABU ya Watford ina azma ya kumsajili, Matej Vydra kwa mkopo kutoka Burnley.
Klabu za Italia, Hispania, Ujerumani na Uturuki pia zinatafuta uhamisho unaowezekana wa muda kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini, Clarets wangependelea uhamisho wa kudumu.(The Athletic).

Declan Rice
WEST Ham imepunguza utathamini wao wa kiungo nyota, Declan Rice.
Wagonga nyundo hao hapo awali waliweka pauni milioni 80 bei ya kuuliza kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England ambaye amekuwa akihusishwa a kuhamia Chelsea.(Goal).

Facundo Pellistri
WINGA wa Manchester United, Facundo Pellistri yuko kwenye mazungumzo ya kuihama klabu hiyo kwa mkopo mwezi huu.
Yoso huyo mwenye umri wa miaka 19 alijiunga na mashetani wekundu kutoka Penarol wakati wa kiangazi, lakini, bado hajaongeza kiwango cha juu.(Goal).

Stephan El Shaarawy
KIUNGO, Stephan El Shaarawy yuko karibu kujiunga tena na Roma.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alitumia miaka mitatu huko Stadio Olimpico kabla ya kumaliza kubadili Shanghai Shenhua mnamo 2019, lakini, sasa anaonekana kurudia hatua zake.( Gazzetta Dello Sport).

David Moyes
KLABU ya West Ham wanapanga kumpa David Moyes kandarasi mpya mwishoni mwa msimu.
Mkataba wa sasa wa meneja wa Scotland unatarajiwa kumalizika mnamo Juni, lakini, wagonga nyundo wanataka kumfunga kwa masharti mapya.(Goal).

Edin Dzeko
JUVENTUS hawapo kwenye mazungumzo ya kumsajili, Edin Dzeko kutoka Roma, licha ya kuongezeka kwa mvutano kati ya mshambuliaji huyo na klabu chake.
Dzeko na wachezaji wenzake walikuwa wameamua kutofanya mazoezi baada ya maandamano wakati wa kuondolewa kwa kocha.(Goal).