Patrick Cutrone
KLABU ya Udinese ipo katika mazungumzo na Wolves kumsaini mchezaji wa Italia, Patrick Cutrone (23), kwa mkopo . Mshambuliaji huyo amekuwa hachezeshwi Molineux tangu kuwasili kwa Willian Jose kutoka Real Sociedad. (Express & Star).

Edin Dzeko
MSHAMBULIAJI, Edin Dzeko, anatarajiwa kuondoka AS Roma baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 raia wa Bosnia kutofautiana na meneja, Paulo Fonseca . (Goal).

Jesse Lingard
MENEJA wa West Ham, David Moyes, anamtaka kiungo wa Manchester United, Jesse Lingard baada ya bosi wa United, Ole Gunnar Solskjaer kukubali kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka kwa mkopo. (Evening Standard).

Gabriel Veron
MANCHESTER United inafanyakazi ya kuzikabili klabu nyengine za Ulaya kama vile Manchester City, Barcelona na Juventus kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 18 raia wa Brazil, Gabriel Veron kutoka Palmeiras. (Sport).

Delle Ali
MENEJA wa Paris St-Germain, Mauricio Pochettino, anatarajia kuungana tena na kiungo, Delle Alli. Maombi matatu ya Mabingwa hao wa Ufaransa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 yamekataliwa, lakini, Pochettino anaungwa mkono na klabu hiyo kuendelea kumnyatia. (The Athletic).

Julian Draxler
KLABU ya PSG wameripotiwa kumtoa kiungo wa kati wa Ujerumani, Julian Draxler (27), kwa mbadala wa mchezaji wa Arsenal na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, Matteo Guendouzi. (L’Equipe).

Charlie Austin
MCHEZAJI wa zamani wa Southampton, Charlie Austin (31), amesema, Manchester United iliamua kumsajili beki wa Sweden, Victor Lindelof (26), badala ya beki wa Liverpool na Uholanzi, Virgil van Dijk mwaka 2017, wakati alipokuwa akiichezea klabu hiyo. (Talksport).

Kaide Gordon
LIVERPOOL inakaribia kuafikia makubaliano ya dau la milioni moja kumsajili kinda wa Derby mwenye umri wa miaka 16, Kaide Gordon. Mchezaji huyo wa timu ya England chini ya umri wa miaka 16 amehusishwa na uhamisho kwenda Manchester United na Tottenham.(Liverpool Echo).

Shkodran Mustafi
KIUNGO, Shkodran Mustafi (28),ameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu kukamilisha kandarasi yake mapema. Mchezaji huyo wa Ujerumani amehusishwa na uhamisho wa kuhamia Lazio na pia amekuwa akizivutia klabu za Ujerumani . (Football.London).

Christian Benteke
KLABU ya Crystal Palace wapo wazi kumuuza, Christian Benteke baada ya kumsaini, Jean-Philippe Mateta.(Goal).

Tyrick Mitchell
BEKI wa Crystal Palace, Tyrick Mitchell, anaivutia Arsenal na washika bunduki hao ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.(Goal).

Kalidou Koulibaly
BEKI wa Napoli, Kalidou Koulibaly bado analengwa na Ole Gunnar Solskjaer huko Manchester United.(Marca).

Virgil van Dijk
LIVERPOOL wanapeana kipaumbele mkataba mpya wa Virgil van Dijk juu ya Mohamed Salah.Van Dijk, ambaye kwa sasa hayuko nje ya uwanja na maumivu ya goti, amebakiza miaka miwili kumaliza mkataba wake wa sasa.(Goal).

Matej Vydra
KLABU ya Watford ina azma ya kumsajili, Matej Vydra kwa mkopo kutoka Burnley.
Klabu za Italia, Hispania, Ujerumani na Uturuki pia zinatafuta uhamisho unaowezekana wa muda kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini, Clarets wangependelea uhamisho wa kudumu.(The Athletic).