Kylian Mbappe
KLABU ya Paris St-Germain itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe (22), mwisho wa msimu huu iwapo mshindi huyo wa Kombe la dunia atakataa kuandikisha kandarasi mpya na miamba hiyo. Klabu ya Liverpool na Real Madrid zina azma ya kumsaini mshambuliaji huyo hatari. (Marca).
Said Benrahma
KLABU ya West Ham itabadilisha kandarasi ya mkopo ya kiungo mshambuliaji wa Algeria, Said Benrahma kutoka Brentford na kumsajili kwa mkataba wa kudumu. West Ham ililipa dau la pauni milioni 4.25 kumnunua mchezaji huyo kwa mkopo na italipa pauni milioni 21.75 kumnunua mchezaji huyo. (Eurosport).
Erling Haaland
CHELSEA ina azma ya kumsaini mshambuliaji wa Borrusia Dortmund mwenye umri wa miaka 20, Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund pamoja na beki wa Bayern Munich, raia wa Austria David Alaba (28). (Goal).
Ainsley Maitland-Niles
BEKI wa Arsenal na England, Ainsley Maitland-Niles (23), yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo ili kupiga jeki nafasi yake ya kushirikishwa katika kikosi cha England cha mashindano ya Ulaya yatakayofanyika majira ya joto. (Mirror).
Thomas Tuchel
MENEJA mpya wa Chelsea, Thomas Tuchel, hana mpango wa kuwasajili wachezaji wapya katika kipindi kilichosalia cha dirisha la uhamisho. (Goal).
Mikel Arteta
MENEJA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema kwamba atafikiria uwezekano wa kuongeza muda wa kandarasi ya mkopo ya Martin Odegaard ili kusalia katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu baada ya kujiunga akitokea Real Madrid. (Times).
Derby Kaide
KLABU ya Liverpool inatarajiwa kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 16 kiungo wa Derby, Kaide Gordon ambaye ameiwakilisha England katika kiwango ha wachezaji wasiozidi umri wa miaka. (Goal).
Jetro Willems
KLABU ya Newcastle United ina azma ya kumsaini tena beki, Jetro Willems baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kuhudumu kwa mkopo katika klabu hiyo msimu uliopita kutoka klabu ya Eintracht Frankfurt. (Chronicle).
Jamal Musiala
UJERUMANI itamuita kiungo wa Bayern Munich, Jamal Musiala (17), katika kikosi kikuu ili kumzuia kuichezea England. Musiala amehudumu miaka minane na Chelsea na England katika timu isiozidi wachezaji wa umri wa miaka 21. (Times).
Marcelo Bielsa
MENEJA wa Leeds United na Argentina, Marcelo Bielsa (65), atasubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kufungua mazungumzo ya kandarasi mpya. (Mirror).
Jeremie Frimpong
KLABU ya Manchester City inatarajia kupata zaidi ya pauni milioni tatu kutoka mauzo ya asilimia 30 kufuatia uhamisho beki wa Uholanzi, Jeremie Frimpong, ambaye aliondoka Celtic na kuhamia Bayer Leverkusen kwa dau la pauni milioni 11.m mapema wiki hii. Frimpong hakukichezea kikosi cha kwanza cha City kabla ya kujiunga na Celtic 2019. (Talksport).
Jean Michael Seri
KIUNGO wa Fulham na Ivory Coast, Jean Michael Seri (29), anatarajiwa kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Bordeaux kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Guardian).
Nathan Collins
KLABU ya Stoke City inataka zaidi ya pauni milioni 15 ili kumuuza beki wake wa kati, Nathan Collins, huku Arsenal na Burnley zikiwa miongoni mwa vigogo vinavyomuwania. (Team Talk).