KAMPALA,UGANDA
KURA zinaendelea kuhesabiwa katika vituo mbalimbali nchini Uganda baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana.
Tume ya Uchaguzi tayari imeanza kutangaza matokeo ya awali katika vituo 300.
Rais aliyeko madarakani Yoweri Museveni anayewania nafasi hiyo kwa muhula wa sita kupitia chama tawala cha NRM anaongoza kwa asilimia 61.3.
Aidha, mgombea wa urais wa upinzani kwa tiketi ya chama cha National Unity Platform, NUP Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amepata asilimia 27.9 ya kura ambazo tayari zimeshahesabiwa.
Kura hizo zinahesabiwa huku hali ya usalama ikiwa tulivu, ingawa huduma ya mtandao wa intaneti bado haijarejea hadi sasa.