LONDON,UINGEREZA

UINGEREZA sasa imekamilisha kuondoka kwake katika Umoja wa Ulaya.

Hii ni baada ya nchi hiyo kuondoka kwenye soko la ndani na umoja wa forodha wa Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema huu ni mwanzo mpya kwa nchi hiyo na mwanzo pia wa uhusiano mpya kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kama rafiki yao mkubwa.

Uingereza iliondoka kwenye Umoja huo rasmi mnamo Januari 31 mwaka uliopita wa 2020 ila imekuwa katika kipindi cha mpito kwa miezi kumi na moja iliyopita hii ikiwa na maana kwamba hakuna kubwa lililobadilika katika utekelezaji.

Makubaliano ya kibiashara ya dakika ya mwisho yalifikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza mkesha wa Krismasi na makubaliano hayo ndiyo yatakayotumika.