ADDIS ABABA, ETHIOPIA

MKUU wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinaadamu katika kambi mbili za wakimbizi kwenye jimbo la kaskazini mwa Ethiopia.

Grandi alisema kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa katika kambi za wakimbizi za Tigray, ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa yalishindwa kufika kutokana na mashambulizi yanayofanywa na jeshi la Ethiopia tangu mwezi Novemba.

Grandi aliipongeza hatua ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kuruhusiwa kwenda kwenye kambi za Mai Aini na Adi Harush na kugawa chakula kwa takriban wakimbizi 25,000 wa Eritrea na kuanza kazi ya kurudisha huduma za maji na afya.

Hata hivyo, Grandi alisema licha ya maombi ya mara kwa mara, bado UNHCR na washirika wake hawajaruhusiwa kuzuru kambi za wakimbizi za Shimelba na Hitsats