NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, amefanya mabadiliko kwenye uteuzi alioufanya Disemba 2020 wa wakuu wa wilaya.

Taarifa kutoka ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar, Hassan Khatib Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Suzan Peter Kunambi na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘B’ Hamida Mussa Khamis.

Wengine ambao wameteuliwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Sadifa Juma Khamis, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Aboud Hassan Mwinyi, Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Rashid Makame Shamsi, na Mkuu wa Wilaya ya Kati, Marina Joel Thomas.

Uteuzi huo pia, Dk. Mwinyi, amemteuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, Mgeni Khatib Yahya, Mkuu wa Wilaya ya Micheweni ni CDR Mohamed Mussa Seif, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake ni Abdalla Rashid Ali na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, ni  Issa Juma Ali.

Wakuu hao wa Wilaya wataapishwa jumatatu saa 10.00 jioni huko Ikulu Mjini Zanzibar.