NA ZAINAB ATUPAE

VIJANA nchini wametakiwa kuyaenzi na kuyadumisha Mapinduzi  matukufu ya Zanzibar  ya mwaka 1964 kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi yao.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Zawadi Hussein Abdalla, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Jimbo la Bububu huko ikiwa ni maadhimisho ya kuelekea kusheherehea mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa  Chuo cha Mwalimu Nyerere.

Alisema Mapinduzi 64, ndio yalioleta uhuru Zanzibar kufanya watu kuishi bila ya kuwa na wasi wasi, kwani kabla wananchi walikuwa wakiishi bila ya uhuru hivyo ni vyema kutumia tunu iliyopo ya Amani.

Aidha aliwataka vijana hao kuendelea kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwani amekuwa na dhamira ya dhati katika kufanya mabadiliko sambamba na kupeleka maendeleo kwa wananchi.

Hivyo aliwataka wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa ya muhali endapo na watakapotakiwa kutoa ushahidi ama kueleza changamoto zilizo ndani ya majimbo yao watoe ili haki ipatikane kwa wakati.

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Rajab Ali Rajab, alisema vijana ndio tegeme la nchi, hivyo ni vyema kuendeleza kufanya kazi za nchi, ili kuweza kuunga mkono viongozi wao na kufikia malengo yaliyowekwa katika nchi.

Nae Khamis Mopeto Khamis, aliwataka vijana hao kuendeleza uzalendo wa nchi yao katika kuipatia mafanikio mbali mbali ya kimaendeleo ya kichumi.

“Tufahamu kuwa bila ya nyinyi kuwa wazalendo na nchi yenu basi munaweza kupoteza kila kitu kilichomo ndani ya nchi hiyo, hivyo munatakiwa nyinyi kuwa kitu kimoja kulinda matunda yenu,”alisema.