NA NASRA MANZI

KAMATI ya Mashindano ya kombe la Mapinduzi  imetangaza bei za viingilio vya uwanjani ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza Januari 5 mwakani.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Khamis Abdalla Said aliwaambia waandishi wa habari kwamba bei ya chini ya viingilio hivyo ni shilingi 2000 kwa jukwaa la urusi.

Akitangaza bei hizo  Khamis alisema kuwa kwa majukwaa ya mzunguuko itakuwa ni shilingi 3000 na kwa VIP itakuwa ni shilingi 5000.

Aidha alisema kuwa bei hizo za viingilio zinaweza kuongezeka wakati wa michezo ya nusu na fainali.

“Kwa kuanza mashindano viingilio vitakua hivyo na tunatarajia wakati wa nusu tutangaza tena”, alisema.

Hata hivyo alisema  katika mashindano ya mara hii wataweka mfumo wa elektroniki wa uuzaji wa tiketi ambapo wananchi watapata kununua mapema na kuendelea kufanya na pirika zao na baadae kuja kuangalia mpira.