ADDIS ABABA, ETHIOPIA

WAZIRI wa Ulinzi wa Sudan ametangaza kuwa wanajeshi wa Ethiopia wamejiweka tayari katika mipaka ya pamoja na Sudan ili kukabiliana na wanajeshi wa nchi hiyo.

Abdulfattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan aliwaambia waandishi wa habari kuwa usalama wa bara la Afrika utakabiliwa na tishio iwapo mapigano yatatokea kati ya Sudan na Ethiopia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan katika jimbo la Darfur Magharibi ilieleza kuwa, watu 83 waliuawa katika mapigano ya kikabila na mashambulizi ya wanamgambo katika mji wa al Janina makao makuu ya mkoa wa Darfur Magharibi, na kuongeza idadi ya majeruhi na kufikia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia alilituhumu jeshi la Sudan kuwa linatumia vibaya mapigano yanayotokea katika eneo la Tigray kaskazini magharibi mwa Ethiopia kwa lengo la kujipenyeza zaidi katika ardhi ya nchi hiyo.

Eneo la mpakani baina ya Ethiopia na Sudan hivi karibuni lilikumbwa na mapigano kati ya wanajeshi wa nchi mbili hizo kwa lengo la kulidhibiti eneo la al Fashaga.