NA ZAINAB ATUPAE

MASHINDANO ya mpira wa miguu yanayoshirikisha timu za Mawizara,Mashirika na Taasisi za Serikali yameendelea kwa kupigwa michezo sita tofauti katika viwanja mbali mbali vya Mkoa wa Mjini Unguja.

Mchezo uliotimua vumbi majira ya saa 2:00 asubuhi uwanja wa Mao Zedong ‘A’ timu ya ZFDA iliondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mahakama.

Maboa ZFDA yaliweka wavuni na Omar Abdalla dakika ya 18 na bao la pili lilifungwa na Makame Khamis dakika ya 47.

Mchezo mwengine Katika uwanja huo huo majira ya saa 4: 00 asubuhi timu ya Afya ilifanikiwa kuifunga Kilimo bao 1-0, bao hilo lilifungwa na Harith Othman dakika ya 14 na kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Mchezo uliotimua vumbi uwanja wa Mao Zedong ‘B’ majira ya saa 2:00 asubuhi timu ya Habara iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ofisi ya Rais na Uwezeshaji.

Bao la Habari liliwekwa wavuni na Ussi Haji Juma dakika ya 12 lilodumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Mchezo uliopigwa uwanja huo huo majira ya 4: 00 asubuhi timu ya ZURA iliondoka na ushindi wa maboa 2-1 dhidi ya Mtakuwimu.

Mabao ya ZURA yalifungwa na Haji Khatib Suleiman dakika ya 12 na bao la pili lilifungwa na Suleyum Mustafa dakika ya 28, huku bao la kufutia machozi la timu ya Mtakuwimu lilifungwa na Ali Mohamed Ali dakika ya 78.

Mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan ‘A’ timu ya Wizara ya Fedha ilipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya Makamu wa pili.

Mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan ‘B’ timu ya ZBS na ZAA zilishishwa kutambiana na kutoka na sare ya kutokufungana.