NA JAMES K MWANAMYOTO-SINGIDA
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amewahimiza Waajiri katika Taasisi za Umma nchini kuwapeleka watumishi wao katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kupatiwa mafunzo bora yatakayowajengea uwezo na kuwaongezea ufanisi kiutendaji ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ndejembi ametoa wito huo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Singida yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani Singida.
Ndejembi amefafanua kuwa, kuna tabia ya baadhi ya Watumishi wa Umma kulewa madaraka ambayo mara kadhaa imekemewa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) George Mkuchika inatokana na watumishi hao kukosa maadili ya kiutumishi, hivyo Chuo cha Utumishi wa Umma ndicho pekee kina uwezo wa kutoa mafunzo yatakayojenga maadili bora kwa Watumishi wa Umma.
Ameongeza kuwa, lengo kuu la kuanzishwa kwa Chuo cha Utumishi wa Umma lilikuwa ni kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao, hivyo ni wajibu wa waajiri wote kukitumia ipasavyo, ili kuondokana na changamoto za kiutendaji na kimaadili zinazowakabili Watumishi wa Umma nchini.
Aidha, Ndejembi amekanusha dhana iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya watu wakidhani Chuo cha Utumishi wa Umma kipo kiushindani dhidi ya Vyuo Vikuu kama UDSM, UDOM, SAUT na Mzumbe na kuongeza kuwa, chuo hicho pia kina jukumu la kutoa mafunzo ya maadili..
Kuhusiana na idadi ndogo ya Watumishi wa Umma wanaopatiwa mafunzo katika Chuo cha Utumishi wa Umma, Ndejembi amehuzunishwa na idadi ndogo ya Watumishi wa Umma 86 tu wa mkoa wa Singida waliopata fursa ya mafunzo katika Kampasi ya Singida wakati chuo kina uwezo wa kutoa mafunzo kwa watumishi wote mkoani humo.
Ndejembi amesema, waajiri wakishirikiana vema na Chuo cha Utumishi wa Umma katika kutoa mafunzo kwa watumishi watakuwa wametekeleza wajibu wa kujenga taifa lenye Watumishi wa Umma wenye tija katika maendeleo ya