NA ZAINAB ATUPAE

KATIBU wa waamuzi wa mpira wa miguu wilaya ya Magharibi ‘B’ Abdul-rahman Mahfoudh, amesema wamejipanga kuchezesha ligi hizo kwa kutimia sheria 17 za mpira wa miguu ili kuondosha migogoro.

Akizungumza na gazeti hili alisema katika kujiandaa huko wametoa mafunzo kwa waamuzi wote ambao watachezesha ligi.

Aidha aliwataka viongozi wa timu ambazo zitashiriki ligi hizo kutoa elimu kwa mashabiki na viongozi,ili kuondosha mikwaruzano inayojitokeza kila mara.

Ahmada Khamis Haji ni Katibu wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Mjini Magharib ,amesema ligi hiyo inatarajiwa kutimua vumbi Januari 3 mwaka 2021 ambapo ufunguzi utakuwa kati ya timu ya Miembeni na Kikwajuni uwanja wa Mao Zedongs ’B’ majira ya saa 10:00 jioni.

Timu 16 zinatarajia kushiriki ligi daraja la pili Mkoa, ambazo ni New City,Gulioni City,Umoja Mbuzini,Maungani United,Kijangwani FC,Mwembeladu,Miembeni,Villa United,Kundemba,Ujamaa,Nyangobo,Bweleo,Kikwajuni,Hawai,Raskazone na Muungano Ranger.