NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo Zanzibar imeshindwa kutamba mbele ya timu inayoundwa na viongozi wa ZFF kwa kufungwa bao 1-0.

Mchezo huo ambao ni amsha amsha ya michuano ya kombe la mapinduzi uliochezwa juzi usiku katika uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo timu hizo ambazo zilitambiana sana zilicheza mchezo mzuri ambao ulitoa msisimko kwa mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo.

Bao hilo la pekee la kombaini ya ZFF liliwekwa kimiyani na mchezaji wake mkongwe Nassor Mwinyi Bwanga katika dakika ya 21.