NA VICTORIA GODFREY

WADAU wa michezo nchini wameombwa kujitokeza kusaidia kufanikisha mashindano ya Kikapu ya  Vijana chini ya umri wa miaka  23 ambayo yamepangwa kufanyika Machi mwaka huu.

Mashindano hayo yanaratibiwa na Water Afrika kwa kushirikiana na Mchenga  Academic.

Akizungumza na gazeti hili,Mratibu wa mashindano hayo, Mohammed Mchenga, alisema lengo ni kuufikisha mchezo wa Kikapu mbele zaidi.

” Maandalizi yanaendelea vizuri na tunatarajia kufanya mashindano yetu kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa vijana kucheza  na kuonyesha vipaji vyao,” alisema Mchenga.

Alisema hadi sasa hawana mdhamini ,hivyo wanaomba wenye mapenzi mema wajitokeze kusaidia ili kufanikisha .