BAMAKO,MALI
WANAJESHI watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Ivory Coast wameuawa eneo la kati nchini Mali.
Umoja wa Mataifa ulisema hayo, ikiwa ni mkasa wa hivi karibuni kukumba taifa hilo linalokumbwa na machafuko la ukanda wa Sahel.
Kulingana na taarifa ya ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, gari la walinda amani hao liligonga bomu la barabarani walipokuwa wakisafiri kwenye barabara inayounganisha mji wa kati Douentza na mji wa kaskazini Timbuktu.
Baadaye wanamgambo walianza kuushambulia msafara wao kwa risasi,Wanajeshi sita waliuawa na wengine sita walijeruhiwa.
Shambulizi hilo ndilo la hivi karibuni katika mzozo ambao ulidumu nchini Mali tangu 2012 wakati wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya Kiislamu waliposhinda uasi uliofanywa na watu waliotaka kujitenga wengi wakiwa wa jamii ya Tuareg kaskazini mwa nchi hiyo.