BEIJING, CHINA
CHINA inasema timu ya wanasayansi kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni itawasili wiki hii huko Wuhan kuanza uchunguzi wake wa asili wa janga la virusi vya corona.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Zhao Lijian alisema kwamba timu hiyo ya washiriki kumi itaondoka kutoka Singapore na kuruka moja kwa moja kuelekea Wuhan, jiji la kati ambalo virusi vya corona iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa 2019.
Hatimaye virusi vilienea karibu kila kona ya ulimwengu, na kusababisha vifo vya zaidi ya milioni 1.9 kati ya karibu maambukizo milioni 91.
China ilitaka kubadilisha hadithi juu ya asili ya virusi,huku maofisa wakishinikiza nadharia ugonjwa uliibuka kwanza katika taifa jengine.
Daktari Mike Ryan,mkuu wa mpango wa dharura wa WHO, aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva kwamba shirika hilo linatafuta majibu ambayo yanaweza kutuokoa katika siku zijazo.