BERLIN,UJERUMANI

HATUA zilizochukuliwa nchini Ujerumani katika juhudi za kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya corona zinaelezwa kushindwa kuleta matokeo yaliyotarajiwa.

Wakati wanasiasa wakuu nchini humo wakitarajiwa kukutana kutathmini matokeo hayo na kupanga mkakati unaofuata, gazeti la Bild limeripoti kuwa wanasiasa hao wana mitazamo tofauti kuhusu muda wa kurefusha vikwazo vilivyopo.

Vikwazo hivyo ambavyo vinajumuisha kufungwa kwa biashara na marufuku ya mikusanyiko, muda wake utamalizika tarehe 10 Januari,lakini baadhi ya wakuu wa majimbo wanataka muda huo urefushwe.

Licha ya vikwazo hivyo, wiki iliyopita Ujerumani ilisajili idadi kubwa zaidi ya maambukizi, na vifo vya watu zaidi ya 1000 kwa muda wa masaa 24.