NA NASRA MANZI

MCHEZAJI wa timu ya Yellow queen inayoshiriki michuano ya soka la wanawake Shuwena Mohamed, ameiomba serikali kuwapa nguvu katika kuinua michezo kwa kuondolewa changamoto zinazowakabili.

Akizungumza na Zanzibar leo hivi karibuni alisema ili soka la wanawake lipige hatua lazima kuwepo na utaratibu wa kusikilizwa changamoto zao.

Hata hivyo alisema michezo imekuwa na fursa nyingi za ajira lakini kwa wanawake kunahitaji mbinu za ziada ambazo zitasaidia kulifikisha sehemu nzuri soka la wanawake.