NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya Soka ya Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali imetinga hatua ya fainali baada ya kuichapa mabao 5-0 Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi na Utawala Bora, katika mashindano ya mawizara,mashirikana na taasisi za serikali.
Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Mao Zedong A. majira ya saa 1:00 asubuhi.
Mabao ya timu ya Wizara yaliwekwa wavuni na Walid Abdi Kombo dakika ya saba,22 na 54, Ali Hassan Ali dakika ya 32 na Juma Masoud dakika 55.
Mchezo uliotimua vumbi uwanja wa Mao Zedong B majira ya saa 1:00 asubuhi timu ya Ofisi ya Makamu wa Pili ilifanikiwa kuendelea na mashindano hayo baada ya kuichapa Wizara ya Habari bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Issa Ramadhan Msenga dakika ya 56 na kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Fainali ya mashindano hayo inatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili ambapo timu ya Wizara ya Elimu na Ofisi ya Makamu wa Pili zikutana uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 jioni.
Mshindi wa kwanza atapata kombe,medali na seti moja ya jezi,mshindi pili atapata medali na seti moja ya jezi.
Kwa upande wa riadha mshindi wa kwanza hadi wa watatu atapatiwa medali na mshindi wa kwanza mchezo wa kuvuta Kamba atazawadiwa kombe na medali na mshindi wa pili atapata medali.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita.