NA ZAINAB ATUPAE

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema itandelea kutatua changamoto za maji kwa wananchi wao na kuhakikisha kila mmoja anapata huduma hiyo bila ya  kikwazo chochote.

Hayo yamelezwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Suleiman Haroub, baada ya kukamilisha zoezi la kufunga mitandao ya maji safi na salama kutoka ZAWA katika shehiya ya Michwanguni wilaya ya Magharibi’B’ Unguja.

Alisema serikali inafanya jitahada kila mara kwa lengo la kuondoa changamoto hiyo ambao ni tatizo la nchi na aliwataka wananchi wa shehiya hiyo kuyatumia vizuri na kulipa maji ili kuondoa usmubufu kwao na ZAWA.

“Shehiya ya Michungwani imekosa maji kwa miaka 20 tumekuwa tukichota maji kwa mtu binafsi ambae alikiwalipisha elfu 20000 kwa kila nyumba ndani ya mwezi mmoja wakati ZAWA unalipa elfu 4000 kweli tulikuwa tunaumia sana,”alisema.

Haji Mussa Haji, Ofisa Mamlaka ya Maji ZAWA Wilaya ya Magharibi’B’ Unguja, alisema tayari wamefungua mitandao yao na kuwataka wananchi  kutumia maji hayo kama inavyotakiwa.

Akitoa shukurani kwa niaba ya wanchi wake Sheha wa shehiya hiyo Faudhia Omar,alimshukuru mwakilishi huyo kwa jitihada alizotoa kwa wananchi wake kwa kuwaondoshea changamo hiyo iliokuwa ikiwasumbua kwa miaka mingi.