HARARE, ZIMBABWE

SERIKALI ya Zimbabwe imetangaza kuwa sheria ya karantini ya nchi nzima imeanza kutekelezwa nchini humo kwa mara nyengine tena kutokana na kuongezeka maambukizi mapya ya corona.

Waziri wa Afya na Makamu wa Rais wa Zimbabwe alisema  kuwa,nchi hiyo imeanza mara moja kutekeleza sheria kali ya karantini ya nchi nzima kwa kuzingatia kuongezeka hivi karibuni maambukizi mapya ya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo.

Takwimu rasmi za karibuni zilizotangazwa na Wizara ya Afya ya Zimbabwe zinaonyesha kuwa,tangu kuenea maambukizi ya corona huko Zimbabwe hadi sasa watu elfu 14 na 84 waliripotiwa kuugua ugonjwa wa Covid-19 nchini humo huku wengine 369 wakifariki kwa ugonjwa huo.

Nchi hiyo ya kusini mwa bara la Afrika mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili ilikumbwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi na ambao ulisababisha kusambaratisha mfumo wa afya ya umma nchini humo.

Kwa mara ya kwanza mwezi Machi mwaka jana Zimbabwe ilikuwa chini ya karantini ya nchi nzima na kuanzia mwezi Mei ilianza kupunguza kwa kiasi kikubwa vizuizi vya karantini kwa nchi nzima.