ANKARA, UTURUKI

RAIS Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amemwondoa madarakani gavana mwingine wa benki kuu ya taifa hilo, Naci Agbal, baada ya kuhudumu miezi michache ofisini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa hilo, Anadolu, mkuu mpya sasa wa benki kuu atakuwa Sahap Kavcioglu, mwanachama wa zamani wa chama tawala cha Erdogan, AKP.

Uamuzi huo umetolewa siku chache baada ya benki kuu ya Uturuki kupandisha kiwango muhimu cha riba kwa alama mbili hadi kufikia asilimia 19.

Gavana mpya Kavciglu atakuwa na jukumu kubwa sasa la kukabiliana na mfumuko wa bei inaotokana na hali ya ongezeko hiyo ya riba.

Hali inayofanana na hiyo ya sasa ilimsababisha Erdogan, Novemba kumuondoa madarakani gavana wa muda mrefu Murat Uysal na kumweka huyu anaemuondoa sasa Agbal.