NA KHAMISUU ABDALLAH

MATAIFA kadhaa duniani yanaungana na Tanzania katika kuomboleza kifo cha mpendwa wetu aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu kwa maradhi ya moyo.

Kifo hicho kimeachasio tu kama kimeacha pengo na huzuni kubwa kwa wananchi wa Tanzania bali hata mataifa ya nje yameguswa pakubwa na msiba huo.

Hayo yamejonesha wazi kwa mabalozi na washirika mbalimbali wa kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa kutokana na kubugunjikwa na machozi na kushindwa kuzuia hisia zao.

Hakika alikuwa ni kiongozi wa watu, mpenda maendeo na amani kwa nchi yake Afrika na dunia kwa ujumla.

Hyati Magufuli alijitoa sadaka na kuutoa moyo wake wote ili kuona watanzania hasa wanyonge wanapata maendeleo.

Alikuwa ni miongoni mwa rais walioweza kuleta maendeleo kwa kipindi kichache alichokaa madarakani kiasi kwamba kila mmoja bila ya kujali tofauti za kisiasa, kidini, kabila wala sehemu anayotoka mtu walikubaliana na hilo.

Katika uongozi wake tulishuhudia Tanzania ikipata mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kufikia uchumi wa kati huku kukishuhudiwa sekta mbalimbali ikiwemo bandari, anga, reli, afya, elimu, barabara na miundombinu nyengine na hata kupewa sifa ya kuitwa Shujaa wa Tanzania.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania kifungu cha 5 kinaeleza kuwa endapo kiti cha urais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uongozi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais wa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.

Hivyo basi kutokana na hali hiyo Tanzania inaandika historia ya mara ya kwanza kupata kiongozi wa juu mwanamke.

Kama alivyokuwa hayati Magufuli, wananchi na washirika wa kimaendeleo pamoja na mabalozi kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuona analeta maendeleo.

Kuwepo kwa kiongozi huyo ni matarajio ya wananchi wengi wa Tanzania wengi kwamba atakuwa mstari wa mbele katika kusimamia maslahi ya wananchi wa Tanzania pamoja na kusimamia haki na stahiki za wananchi wote wanyonge.

Matumaini ya watanzania Rais Samia atakuwa jemedari wao, raisi wao na amiri jeshi mkuu wa nchi, rais mwema, mchapa kazi na mama ambae atalea taifa la Tanzania na kuendelea kudumisha taifa la Tanzania