BEIJING, CHINA

NAIBU Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Afrika wa Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ahunna Eziakonwa, amesema nchi za Afrika zinaweza kujifunza uzoefu wa China katika kupambana na umaskini.

Eziakonwa alisema hayo wakati wa kusainiwa kwa makubaliano kati ya UNDP na eneo la biashara huria la Afrika (AfCFTA), yenye lengo la kuhimiza biashara barani Afrika.

Alisema Afrika inaweza kulimaliza tatizo la umasikini kama itajifunza namna China ilivyoweza kukabiliana na tatizo la kulimaliza.

“Tumeina China namna ilivyopambana na kuimaliza changamoto ya umasikini kwa wananchi wake, Afrika inalo la kujifunza kwenye mafanikio yaliyofiiwa na China”, alisema Eziakonwa.

Akizungumzia mktaba huo, Eziakonwa alisema utakuwa kichocheo cha kufufua maendeleo ya kiuchumi na kijamii baada ya msukosuko wa janga la COVID-19, na kama kichocheo cha maendeleo endelevu kwa mambo ya wanawake na watoto.

Akizungumzia mchango unaoweza kutokea na China kwenye eneo la biashara huria la Afrika, Eziakonwa alisema China imeweza kuwaondoa watu wake milioni 700 kutoka kwenye lindi la umaskini na Afrika inaweza kujifunza kwa ilichofanya China.