MOGADISHU, SOMALIA 

KUNDI la kigaidi la wanamgambo la al-Shabaab limeripotiwa kufanya mashambulizi dhidi ya jeshi la Somalia katika mkoa wa Lower Shabelle, maofisa wa mkoa walithibitisha.

Mashambulizi hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa kumi alfajiri kwa saa za Somalia, yakilenga kambi za jeshi katika miji ya Barire na Awdhegle kusini mwa Somalia.

Vituo vya uendeshaji vilivyo mstari wa mbele vinavyosimamiwa na jeshi la Somalia ili kulinda madaraja kadhaa yaliyoko kwenye mto Shabelle ambavyo mamlaka inasema ni muhimu katika kuzuia gari yanayo beba vifaa vya miripuko kuingia Mogadishu.

Mashambulizi yalianza na gari lenye mabomu ya kujitoa muhanga katika kambi mbili za jeshi, yakifuatiwa na shambulizi la ardhini, maofisa wa mkoa walisema.

Gavana wa mkoa wa Lower Shabelle, Abdulkadir Mohamed Nur Siidi alithibitisha kutokea mashambulizi hayo na kueleza kuwa wanamgamgambo hao  walirusha mabomu katika vijiji jirani vya Sabiid na Anole.

Katika miaka ya karibuni, jeshi la Somalia, kwenye operesheni za pamoja na tume ya ulinzi wa amani katika kanda hiyo, vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia, au AMISOM vimeweza kuvikamata tena vijiji hivyo ambavyo hapo awali vilikuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo wa al-Shabaab.

Majeshi ya serikali yamefanikiwa kuzima shambulizi huko Awdhegle na kulihami daraja kuu linalotumiwa na raia na wanajeshi, lakini kulikuwa na mapigano makali katika mji wa Barire, maafisa wameongeza.

Kikundi cha wanamgambo wa Al-Shabaab kimedai kuharibu kituo cha kijeshi cha Barire, ofisa mmoja wa mkoa, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu hana ruhusa ya kuongea na vyombo vya habari, amesema Barire imeathiriwa na shambulizi hilo.

Maofisa wawili wamesema wapiganaji hao waliingia katika kambi ya kijeshi ya Barire bila ya kutoa maelezo zaidi. Wapiganaji hao hivi sasa wamefurushwa kutoka Barire, afisa mmoja ameeleza.