NA MARYAM HASSAN

MAHAKAMA ya wilaya Mwera imemtoza faini ya shilingi 280,000 dereva aliyesababisa hasara kwa kuugonga ukuta wa Chuo cha Utawala wa Umma (IPA), na gari  iliyokuwa inaendeshwa na Shambul Salum Meru

Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu Taki Abdalla Habibu wa mahakama ya wilaya Mwera na kueleza, kwa adhabu hiyo ya kuendesha chombo cha moto bila ya kuwa na hadhari na kumtaka kulipa faini ya shilingi 100,000.

Mbali na adhabu hiyo, pia alitakiwa lipa faini ya shilingi 100,000 kwa kosa la kuendesha chombo cha moto barabarani bila ya hadhari na kusabbaisha kuigonga gari iliyokuwa inaendeshwa na Shambul Salum Meru.

Hakimu taki alisema, kwa kosa kuendesha chombo cha moto ikiwa hana leseni ya udereva alitamtaka kulipa faini ya shilingi 80,000.

Hivyo mshitakiwa ametakiwa kulipa faini ya shilingi 280,000 kwa makosa yote matatu na akishindwa atumikie Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi sita kwa kosa.

Dereva huyo ni Khamis Ali Said (27) mkaazi wa Melinne, ambae anadaiwa kutenda kosa la kwanza Disemba 16 mwaka jana majira ya saa 9:45 za jioni huko Tunguu wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.

Akiwa dereva wa gari yenye nambari za usajili Z815 KN wakati huo akitokea Mjini kuelekea Tunguu alipofika IPA, aliendesha chombo hicho bila ya hadhari na kwa uzembe na kupelekea kuonga gari yenye nambari za usajili Z788 JQ.

Gari hiyo ilikuwa ikindeshwa na dereva Shambul Salum Meru na kupelekea kusababisha hasara kwa gari hiyo kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Aidha kosa la pili kwa mshitakiwa huyo ni kuendesha chombo cha moto barabarani bila ya kuwa na hadhari na kwa uzembe, kosa ambalo ni kunyume na kifungu cha 117 sheria nambari 7 ya mwaka 2003 sheria za Zanzibar.

Mshitakiwa anadaiwa kuendesha chombo hicho kwa uzembe na kusababisha kuugonga ukuta wa Chuo cha Utawala wa Umma na kupelekea hasara kwenye chuo hicho.