NA VICTORIA GODFREY
BONANZA la michezo ya mpira wa Wavu Mikono litafanyika leo Aprili 9 Mbweni JKT,Dar es Salaam.
Mratibu wa mashindano hayo Papa Hamis Papa,alisema tayari klabu sita zitashiriki bonanza hilo.
Alizitaja klabu hizo kwa mpira wa Wavu ni JKT,Chui (wanawake na wanaume),Jeshi Stars (wanaume) Magereza (wanawake),huku Mpira wa Mikono ni Victoria, Ukonga JKT zote wanawake na wanaume.
“Maandalizi yanaendelea na matarajio yetu tutapata tulichokusudia kwani kila mmoja atajiandaa ili kuibuka na ushindi,” alisema Papaa.
Alisema lengo ni kuhakikisha wanashiriki ili kujenga ushirikiano na Umoja kupitia bonanza hilo.