NAIROBI, KENYA

BAADHI ya watu maarufu nchini Kenya wamethibitisha kupokea chanjo ya kudhibiti ugonjwa wa corona ya Sputnik V iliyotengezwa nchini Urusi.

Watu walithibitisha kuwa wameshapatiwa chanjo hiyo ambayo serikali ya Kenya, ya serikali ya Kenya bado haijaidhinisha matumizi yake.

Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa hasa usalama wa afya waliotumia chanjo hiyo na ufanisi wake katika kudhibiti ugonjwa huo.

Hapo juzi ubalozi wa Urusi nchini humo ulieleza kuwa hauhusiki na uingizwaji wa chanjo hiyo.

Ubalozi huo ulifafanua kwamba chanjo ya Sputnik V iliingizwa nchini Kenya na taasisi binafsi kwa lengo la kibiashara.

Kupitia taarifa rasmi ubalozi huo zimezitaka taasisi zinazoingiza chanjo hiyo lazima wafuate masharti yote yaliyotolewa na mamlaka ya Kenya.

Dokta Mercy Mwangani, ni ofisa msimamizi katika wizara ya afya amenukuliwa na vyombo vya habari akisema wamepokea taarifa kuingia nchini kwa chanjo ya Sputnik V.

“Tuna mkataba unaoeleza majukumu ya kila anayehusika katika usambazaji wa chanjo hiyo lakini haujawasilishwa kwenye bodi ya wafamasia, hii ina maana chanjo hiyo haijaidhinishwa”, alisema.

Miongoni mwa waliopokea chanjo hiyo ni mawakili wakichapisha kwenye mitandao picha za zoezi zima la kupewa chanjo walivyokuwa wakipewa.