Ismaila Soro
KLABU ya Tottenham wanamuwinda kiungo wa Celtic raia wa Ivory Coast, Ismaila Soro. (Mail).
Arsene Wenger
KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anajiandaa kujiunga na mpango wa kuinunua klabu hiyo pamoja bilionea, Daniel Ek na wachezaji wake watatu wa zamani. (BeIN Sports).
Ibrahima Konate
LIVERPOOL bado wana mipango ya kumsajili beki wa RB Leipzig, Ibrahima Konate (21), kwa dau la pauni milioni 40 mwishoni mwa msimu, licha klabu hiyo kutangaza hasara ya pauni milioni 46 kabla ya kodi. (Mail).
Hansi Flick
CHAMA cha Soka cha Ujerumani kinatarajiwa kuanza mazungumzo na kocha anayeondoka katika klabu ya Bayern Munich, Hansi Flick, ili kuchukua nafasi ya Joachim Low kama kocha wa timu ya taifa hilo. (90min).
Brendan Rodgers
KOCHA wa Leicester City, Brendan Rodgers, hana mpango wa kuhamia Tottenham kuchukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kutimuliwa, Jose Mourinho. (Sky Sports).
Jesse Lingard
WINGA wa England, Jesse Lingard (28), atapigania kuihama klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu pale mkataba wake wa mkopo na West Ham utakapokatika. (Eurosport).
Sergio Aguero
KLABU ya Inter Milan imeingia katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji, Sergio Aguero (32), ambaye ameshatangaza kuondoka Manchester City mara baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu. (Caciomercato).
Jonathan David
MSHAMBULIAJI wa Lille raia wa Canada, Jonathan David (21), yupo katika mawindo ya Manchester United na Arsenal. (Fichajes.net).
Khvicha Kvaratskhelia
KLABU ya Leeds United wamefanya mazungumzo juu ya kumsajili winga wa Rubin Kazan raia wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia (20). (Football Fancast).
Davy Propper
KIUNGO wa Brighton raia wa Uholanzi, Davy Propper (29), anawindwa na klabu yake ya zamani ya Uholanzi, PSV Eindhoven. (The Argus).