NA ZAINAB ATUPAE

LIGI soka daraja la Kwanza Kanda ya Pemba inatarajiwa kutimua vumbi Aprili 8 kwa kuchezwa michezo miwili tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba iliotolewa na uongozi wa chama hicho katika uwanja wa Gombani majira ya saa 8 :00 mchana timu ya Chake Chake itakutana na Dot Mound wakati wa saa 10:00 jioni timu ya Jamhuri itacheza na Yosso Boys.

Katika uwanja wa FFU Finya majira ya saa 10:00 jioni timu ya Maendeleo Mantar itatoana majasho na Libakuza.

Siku ya Ijumaa kutapigwa mchezo mmoja majira saa 10:00 jioni uwanja wa FFU Finya timu ya Maji Makali itacheza na New Stown.

Siku ya Jumamosi ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa michezo miwili uwanja wa Gombani majira ya saa 10:00 jioni timu ya Mwenge itacheza na Afrikana,huku uwanja wa FFU Finya majira ya saa 10:00 jioni timu ya Kizimbani itacheza na Umeme.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa kuchezwa michezo mitatu ambapo uwanja wa Gombani majira ya saa 10:00 jioni timu ya Jamhuri itacheza na Chake Chake,huku uwanja wa FFU Finya timu ya Afrikana itakutana na Dot Mound.

Mchezo mwengine utachezwa uwanja wa Gombani majira ya saa 8:00 mchana Yosso Boys itavutana na Kizimbani.