NA ZAINAB ATUPAE

LIGI daraja la tatu wilaya ya Magharibi ’B’ Unguja imeendelea kutimua vumbi kwa kuchezwa michezo mbali mbali katika viwanja tofauti ndani ya wilaya hiyo.

Mchezo uliotimua vumbi uwanja wa Kiembe Samaki majira ya saa 8:00 mchana Small Really iliondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tomondo FC.

Uwanja huo huo majira ya saa 10 :00 jioni timu ya Mitondooni FC na Young Killer ziligawana pointi baada ya kutoka na sare ya mabao 2-2.

Uwanja wa Dimani majira ya saa 10 :00 jioni timu ya Kimara ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Small Fight.

Ligi hiyo itendelea tena baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani.