BUJUMBURA, BURUNDI
MAZUNGUMZO baina ya serikali ya Burundi na Umoja wa Ulaya yanaendelea vizuri ambapo huenda Umoja huo ukaiondolea vikwazo nchi hiyo mnamo mwishoni mwa mwaka huu.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Burundi, Albert Shingiro alisema mchakato wa mazungumzo baina Burundi na Umoja huo yanaendelea mazuri kiazi cha kulea matumaini makubwa kwa taifa hilo kuondolewa vikwazo.
Shingiro alisema wamefanya vikao viwili na mwawakilishi wa umoja wa Ulaya nchini humo Claude Bochu mazungumzo ambayo pia yaliwashirikisha mabalozi wa wa Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani waliopo nchini humo.
Waziri huyo alibainisha kuwa mazungumzo zaidi yaendelea mwezi Juni ambapo ataongoza ujumbe wa nchi hiyo kwenda kwenye mazungumzo hayo yatakyofanyika barani Ulaya.
Umoja wa Ulaya uliwaekea vikwazo baadhi ya viongozi wa siasa nchini humo kufuatia kile kilichoitwa ukandamizaji na uvunjwaji wa haki za binaadamu zilizotokea mwaka 2015 baada kufeli jaribio la mapinduzi lililofeli.
Aidha Burundi ilikabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu hasa kwa wapinzani nchini humo waliokuwa wakipinga rais wa zamani wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kulazimisha kuingia madarakani kwa muhula wa tatu ambao ni kinyume cha katiba.
Inaelezwa kuwa katika ukandamizaji huo wa haki za binaadamu na matumizi ya nguvu kiasi cha watu 1,200 walifariki na wengine wapatao 400,000 kukimbia nchi hiyo kutafuta hifadhi nje ya nchi.