B

RUSSELS, UBELGIJI 

SHIRIKA la polisi la Ulaya, Europol limetowa ripoti yake inayosema kwamba uhalifu wa kupangwa unaenea zaidi katika maeneo yote ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Tathmini ya ripoti hiyo iliyotolewa mjini Lisbon, nchini Ureno imeonesha kwamba kitisho kimeongezeka kuliko wakati mwingine, kwa nchi za Umoja wa Ulaya na raia wake.

Aidha imeelezwa katika ripoti hiyo kwamba kuna kitisho kikubwa kinachoonesha kwamba wahalifu pia watatumia janga la virusi vya corona na athari zake za muda mrefu za kiuchumi na kijamii kuwalenga raia, biashara na maeneo ya umma.

Ripoti hiyo imeandikwa baada ya kufanyika uchunguzi ulioangazia maelfu ya visa na data zilizotolewa na wachunguzi na idara za usalama kote katika Umoja wa Ulaya.

Zaidi ya asilimia 80 ya mitandao ya uhalifu imegundulika inatumia mifumo halali ya biashara na asilimia 60 ya magenge yanatumia ufisadi kama njia ya kuendeleza biashara zao.